Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 19, 2016

Wakimbizi 200 wa Boko Haram wafa kwa njaa

MTEULE THE BEST     Watu 200 waliokimbia kutoka kwa maeneo yaliyovamiwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram nchini Nigeria, wamefariki kutokana na baa la njaa na ukosefu wa maji. Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka- MSF, linasema kuwa vifo hivyo viltokea mwezi uliopita, katika kambi moja duni ya wakimbizi wa ndani kwa ndani, Kaskazini- Mashariki mwa nchi hiyo. MSF linasema kuwa uhaba huo wa vyakula na maji unatishia maisha ya wakimbizi zaidi wa ndani kwa ndani katika kambi ya wakimbizi ya Bama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kambi hiyo yamkini inawakimbizi takriban elfu 20,000 hivi.   Umoja wa mataifa unakisia kuwa machafuko yaliyosababishwa na wanamgambo wa Boko Haram maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria yamesababisha watu milioni 2 kutoroka makwao. ...

JE KIWANGO CHA ROONEY KIMESHUKA AMA KIMEPANDA

MTEULE THE BEST   JE KIWANGO CHA ROONEY  KIMESHUKA AMA KIMEPANDA KULINGANISHA MIAKA ILIYOPITA   Unamkumbuka Rooney wa miaka  7 iliyopita? Si huyu tena Rooney kabadilika,Hana uwezo ule tena wa miaka 7 iliyopita na kufanya awe kipenzi cha mashabiki wa Manchester united.Rooney hana jipya kwa sasa pale Manchester united lakini uwepo wake una faida kubwa klabuni hapo. Mwaka 2002 Katika mechi kati ya Arsenal dhidi ya Everton Rooney aliifungia Everton goli la ushindi akiwa na miaka 17 siku 7 kabla ya kutimiza miaka hiyo 17.Goli hilo lilivunja rekodi ya arsenal ya kutokufungwa katika michezo 30. Kama isingekuwa dau dogo la Newcastle huenda Rooney angetua St James park lakini Dau la £25.6 lilimpeleka katika viunga vya old Trafford ndio kwanza ana umri wa miaka 18. Unajua kwa nini alitua Manchester united? Viongozi na mkufunzi wa Manchester united Alex Ferguson waligundua Rooney alikuwa ni mchezaji aliyekamilika.Usibishe. Katika umri wa miaka 18 kwen...

SHERIA YA MUNGU

MTEULE THE BEST   TUMSIFU YESU KRISTO WAPEDWA KATIKA BWANA MTEULE G KAHANGILE LEO SOMO LINATOKA ZABURI 19:7-14  MADA: SHERIA YA MUNGU Sheria ya MWENYEZI-MUNGU ni kamilifu humpa mtu uhai mpya; masharti ya MWENYEZI-MUNGUni thabiti, huwapa hekima wasio na makuu  Kanuni za MWENYEZI-MUNGU ni sawa hufurahisha moyo  amri ya MWENYEZI-MUNGUni safi humwelimisha mtu   kumcha MWENYEZI-MUNGUni jambo jema na la kudumu milele ; maagizo ya MWENYEZI-MUNGUni sawa yote ni ya haki kabisa  Yatamanika kuliko dhahabu kuliko dhahabu safi kabisa  Nimatamu kuluko asali kuliko asali safi kabisa Yanifunza mimi mtumishi wako kuyafuata kwani letea tuzo kubwa  Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe ?  Ee MUNGU niepushe  na makosa nisiyojua Unikinge mimi mtumishi wako na makosa ya makusudi usikubali hayo yanitawale. Hapo nitakuwa mkamilifu wala stakuwa na hatia ya kosa kubwa Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu yakub...

Ahukumiwa kwa kutembea kutoka Ufaransa hadi Uingereza

MTEULE THE BEST   Mwanamame mmoja raia wa Sudan amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na mahakama moja nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kutembea kwa miguuu kutoka nchini Ufaransa hadi Uingereza akipitia kwa reli Abdul Rahman Haroun, ambaye alikiri mashtaka hayo alikuwa amepewa hifadhi nchini Uingereza mwaka uliopita. Mwanamme huyo wa umri wa miaka 40 anaaminika kutembea umbali wa kilomita 50 kutoka Calaisin nchini Ufaransa, hadi Folkestone nchini Uingereza kabla ya kupatikana tarehe 4 mwezi Agosti mwaka uliopita. Hata hivyo hawezi kufungwa jela kutoka na kipindi ambacho tayari amekuwa kizuizini.  

Ndovu auawa na umeme Uganda

MTEULE THE BEST     Ndovu mmoja katika mbuga ya wanyama pori ya Queen Elizabeth nchini Uganda, amefariki baada ya kupigwa na umeme, kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la Daily Monitor. Shirika la wanyamapori nchini humo (UWA) linasema kuwa msoga wa ndovu huyo, ulipatikana asubuhi kwenye nyaya za umeme zinazounganisha umeme na transifoma moja. Ukuta wa nyaya uliokuwa ukizunguka transifoma hiyo, ulikuwa umeharibiwa wakati ndovu huyo alijaribu uvuka.

David Rudisha ni 'afande' Kenya

MTEULE THE BEST     Je wajua kuwa bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 za wanaume David rudisha ni afisa mkuu wa polisi nchini Kenya? maelfu ya mashabiki wake walipigwa na butwaa alipochapisha picha yake akiwa amevalia sare rasmi ya kikosi cha utumishi kwa wote katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.   Bingwa huyo na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 800 kwa upande wa wanaume ni afisa mkuu wa polisi Picha hiyo inayomuonesha akiwa amevalia sare ya kikosi cha polisi inadhihirisha kuwa ni afisa wa ngazi ya juu. Sio aghalabu kuwa bingwa huyo na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 800 kwa upande wa wanaume ni afisa polisi, asilimia kubwa ya wanariadha wakenya ni maafisa wa idara mbali mbali za vikosi vya ulinzi.   ...

Victor Wanyama ajiunga na Tottenham Hotspur

MTEULE THE BEST   Victor Wanyama ajiunga na Tottenham Hotspur   Tottenham Hotspur imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Southampton mkenya Victor Wanyama kwa kima cha pauni milioni 11. Inaaminika kuwa wanyama mwenye umri wa miaka 24, ambaye alijiunga na Southampton akitokea Celtic mwezi Julai mwaka 2013 kwa pauni milioni 12.5, kwa sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiafya. Sasa wanyama ataungana na meneja wake wa zamani Maurico Pochettino.  

Tanzania kutengeneza ndege aina ya helikopta

MTEULE THE BEST     Tanzania kutengeneza ndege aina ya helikopta   Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linaunda ndege. Gazeti la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi. Gazeti la Zambia, Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo. Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka. Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News.  

Ashtakiwa kumtusi Magufuli katika WhatsApp

MTEULE THE BEST   Ashtakiwa kumtusi Magufuli katika WhatsApp   Raia mmoja wa Tanzania amefunguliwa mashtaka kutokana na ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo anadaiwa kumtusi Rais John Pombe Magufuli. Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni. Ni mtu wa pili kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa tuhuma za kumtusi rais. Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanza kutekelezwa mwaka uliopta. Kyaruzi anadaiwa kuandika: "'Kwani rais Magufuli hana washauri? hashauriki? Ama ni mjinga tu? Ni Mpumbavu sana. Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?.  

Marekani yapambana na moto wa msituni California

MTEULE THE BEST   Marekani yapambana na moto wa msituni California Wazima moto kusini mwa California nchini Marekani wanajaribu kuzima moto ambao umewalazimu mamia ya watu kuhama makwao. Maafisa kutoka shirika shirika la Cal-Fire, wanasema kwa miundo msingi kadhaa katika eneo la Santa Barbara, imetishiwa na moto huo unaochochewa na upepo mkali. Wataalamu wanaonya kuwa hali ya kiangazi pia imechangia moto huo kuenea zaidi hadi maeneo ya milima yaliyo jimbo la Los Angeles.