MTEULE THE BEST
JE KIWANGO CHA ROONEY KIMESHUKA AMA KIMEPANDA KULINGANISHA MIAKA ILIYOPITA
Unamkumbuka Rooney wa miaka 7 iliyopita? Si huyu tena
Rooney kabadilika,Hana uwezo ule tena wa miaka 7 iliyopita na kufanya
awe kipenzi cha mashabiki wa Manchester united.Rooney hana jipya kwa
sasa pale Manchester united lakini uwepo wake una faida kubwa klabuni
hapo.
Mwaka 2002 Katika mechi kati ya Arsenal dhidi ya Everton
Rooney aliifungia Everton goli la ushindi akiwa na miaka 17 siku 7 kabla
ya kutimiza miaka hiyo 17.Goli hilo lilivunja rekodi ya arsenal ya
kutokufungwa katika michezo 30.
Kama isingekuwa dau dogo la Newcastle huenda Rooney angetua
St James park lakini Dau la £25.6 lilimpeleka katika viunga vya old
Trafford ndio kwanza ana umri wa miaka 18.
Unajua kwa nini alitua Manchester united? Viongozi na
mkufunzi wa Manchester united Alex Ferguson waligundua Rooney alikuwa ni
mchezaji aliyekamilika.Usibishe.
Katika umri wa miaka 18 kwenye michuano ya mabingwa ulaya
akifunga hat trick dhidi ya fernebahce. Utagundua alikuwa na vitu adimu.
Kwa bahati Rooney katwaa kila kitu katika ngazi ya klabu na
pia katwaa tuzo nyingi binafsi kama Golden boy mwaka 2004 Kutokana na
ubora wake kwa kipindi hicho
Nguvu za miguuni,Akili,Ubunifu na ujuzi ndiyo vitu ambavyo
Rooney ilikuwa silaha yake na kumfanya awe na uwezo wa kufunga popote
katika dimba.Bado Rooney alikuwa na uwezo wa kuwasaidia washambuliaji
(Supporting forward) kutokana na uwezo wa kupiga pasi zenye ubora na
kucheza kama kitimu.
Miaka ikasonga na kusonga Rooney aliendelea kuwa kioo cha
mafanikio ya Manchester united kutokana na uwezo wake wa kujitolewa na
kuwa kiongozi uwanjani,alifunga magoli mazuri mfano Tiki taka dhidi ya
Manchester city alikuwa na miaka 26.
Ukweli unabaki pale Pale Rooney yule si huyu hana tena
uwezo wa kuwasumbua mabeki,kukimbia walau hata kufunga magoli sehemu
yeyote ya uwanja kutokana na uwezo wake kupungua alitumika mno enzi za
ubora wake na kuvunja rekodi kadha wa kadha kwenye klabu na taifa.
Rooney hapendelei kutumika kama kiungo bado anahitaji
kuvunja rekodi na kuwa mfungaji bora wa Manchester united lakini uwezo
wake kwa sasa unamruhusu kutumika katika eneo moja nalo ni kiungo.
Ferguson,Moyes na hata Louis van gaal huwa walitumia na
sasa lvg anamtumia kama kiungo kutokana na walijua kuwa kwa sasa Rooney
anauwezo wa kukupa kitu kimoja tu miguuni mwake nazo ni pasi ndefu na
fupi.pia bado kwa umri wa Rooney miaka 31 hawezi tena kucheza katika
ubora ule dhidi ya mabeki wa timu pinzani anahitajika kucheza katika
eneo ambalo halina presha (Kiungo).
Morgan schneiderlin, Herrera,Bastian schweinsteiger,Fellain
viungo wote hao wana sifa moja kukaba lakini sio kupiga pasi za uhakika
(Ndefu na fupi) ndio maana Leo De Gea huwezi kuwafunga Manchester
united goli 4 wana sifa ya kuwa ni viungo wakabaji.
Tofauti kubwa ya viungo hao na Rooney ni kuwa Uwezo wa
miguu ya Rooney wa kupiga pasi ndefu na fupi unamfanya Rooney alitawale
eneo la kiungo.Hilo ndilo eneo pekee analoweza kucheza bila presha walau
kwa miaka 3 ijayo.Ndio maana David Moyes aliishawahi kumtumia katika
eneo hilo na sasa Lvg.
Majeraha na umri ni vikwazo kwa Rooney hawezi kurejea tena kwenye kilel cha mafanikio.
Si yule wa miaka 7 kwa sasa eneo pekee la Rooney ni kucheza
hapo kiungo ndipo anaweza kurefusha miaka 3 ijayo katika soka lakini
kuwa Mshambuliaji kwa sasa atakuwa anapoteza muda tu.
Maoni