MTEULE THE BEST
Ndovu mmoja katika mbuga ya wanyama
pori ya Queen Elizabeth nchini Uganda, amefariki baada ya kupigwa na
umeme, kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la Daily Monitor.
Shirika
la wanyamapori nchini humo (UWA) linasema kuwa msoga wa ndovu huyo,
ulipatikana asubuhi kwenye nyaya za umeme zinazounganisha umeme na
transifoma moja.Ukuta wa nyaya uliokuwa ukizunguka transifoma hiyo, ulikuwa umeharibiwa wakati ndovu huyo alijaribu uvuka.
Maoni