Rais wa Urusi Vladimir Putin amemwambia kansela Angela Merkel kwamba gesi ya asili ya Urusi inaweza kupelekwa kwenye nchi jirani ya Ukraine iwapo yatakuwepo manufaa ya kiuchumi kwa Urusi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye mazungumzo yao wamejadiliana kuhusu mgogoro wa nchini Ukraine, wakati ambapo Urusi inaongeza ukubwa wa bomba lake la gesi ya asili kwenda moja kwa moja hadi nchini Ujerumani, bila kupitia Ukraine. Rais Putin na Waziri wake Mkuu Dmitry Medvedev walimkaribisha Kansela Merkel katika makao ya rais ya majira ya kiangazi yaliyopo katika jiji la kusini mwa Urusi la Sochi, kansela Merkel ndiye aliyeongoza vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi wakati nchi hiyo ilipolitwaa jimbo la Crimea miaka minne iliyopita. Lakini katika miezi ya hivi karibuni, Ujerumani ilitoa idhini yake kwa Urusi kuweza kutanua bomba lake la gesi la Nord Stream, ambalo litasafirisha gesi ya asili hadi nchini Ujerumani licha ya Ukraine kuupinga mra...