Ndege ya Urusi ilipigwa picha karibu na uwanja wa ndege wa Caracas Jumapili Ndege mbili za kijeshi za Urusi zilitua katika uwanja mkuu wa ndege wa Venezuela Jumamosi, zikiripotiwa kuwa na makumi kadhaa ya wanajeshi na kiwango kikubwa cha zana. Ndege hizo zilitumwa "kutekeleza mkataba wa kijeshi wa kiufundi ", limeripoti shirika la habari la Urusi Sputnik limeripoti. Javier Mayorca, mwandishi wa habari wa Venezuela, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba aliona wanajeshi wapatao 100 na tani 35 za vifaa vikishushwa kwenye ndege. Hii inakuja miezi mitatu baada ya nchi hizo mbili kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi. Urusi imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Venezuela, ikiikopesha nchi hiyo iliyoko Amerika Kusini mabilioni ya dola na kusaidia sekta yake ya mafuta na jeshi. Urusi pia ilikuwa wazi kupinga hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo serikali ya rais wa Venezuelan Nicolás Maduro. Bwana Mayorca alisema kwenye Twitter ndege ya kijeshi ya Urusi ya mizig...