Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mzozo wa Venezuela: Ndege ya Kijeshi ya urusi yatua karibu na Caracas




Ndege ya Urusi ilipigwa picha karibu na uwanja wa ndege wa Caracas Jumapili

Ndege mbili za kijeshi za Urusi zilitua katika uwanja mkuu wa ndege wa Venezuela Jumamosi, zikiripotiwa kuwa na makumi kadhaa ya wanajeshi na kiwango kikubwa cha zana.


Ndege hizo zilitumwa "kutekeleza mkataba wa kijeshi wa kiufundi ", limeripoti shirika la habari la Urusi Sputnik limeripoti.

Javier Mayorca, mwandishi wa habari wa Venezuela, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba aliona wanajeshi wapatao 100 na tani 35 za vifaa vikishushwa kwenye ndege.


Hii inakuja miezi mitatu baada ya nchi hizo mbili kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Urusi imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Venezuela, ikiikopesha nchi hiyo iliyoko Amerika Kusini mabilioni ya dola na kusaidia sekta yake ya mafuta na jeshi.

Urusi pia ilikuwa wazi kupinga hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo serikali ya rais wa Venezuelan NicolƔs Maduro.

Bwana Mayorca alisema kwenye Twitter ndege ya kijeshi ya Urusi ya mizigo Antonov-124 na ndege ndogo aina ya Jet zilitua karibu na mji mkuu Caracas siku ya Jumamosi.

Alisema kuwa Generali wa Urusi Vasily Tonkoshkurov aliwaongoza wanajeshi hao walipokuwa wakitoka ndani ya ndege.

Ndege ya kijeshi ikiwa na nembo ya bendera ya Urusi inaonekana kwenye uwanja wa ndege Jumapili. Picha kwenye mitandao ya habari ya kijamiipia zilionyesha wanajeshi wamekusanyika katika uwanja wa ndege.

More Russian soldiers unload in #Venezuela to help prop up Pres. #Maduro. The Ilyushin IL-62M is used to carry military personnel and frequently flies troops from #Russia to Syria -- indeed it stopped in #Syria on its way from Russia to #Caracaspic.twitter.com/YfU2SnZacJ


ā€” Prof. Steve Hanke (@steve_hanke) 24 Machi 2019


Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @steve_hanke

Mahusiano baina ya Moscow na Venezuela yameimarika katika miezi ya hivi karibuni , wakati uhusiano kati ya Marekani na Venezuela ukiwa mbaya zaidi. Mwezi Disemba, Urusi ilituma ndege za kijeshi aina ya Jet nchini Venezuela kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi.

Mzozo wa kisiasa Venezuela wageuka mgogoro wa kimataifa


Urusi iliyalaani mataifa mengine ya kigeni kwa kumuunga mkono kiongozi wa upinzani wa Venezuela Juan GuaidĆ³, ambaye alijitangaza kama rais wa mpito mwezi Januari.

Rais Maduro amemshutumu Bwana GuaidĆ³ kujaribu kupanga mapinduzi dhidi yake kwa usaidizi wa "Wavamizi wa Marekani".

Utawala wa Kremlin uliunga mkono kauli hiyo ,ukimshutumu Bwana GuaidĆ³ kwa "kujaribu kunyakua mamlaka kinyume cha sheria " akiungwa mkono na Marekani na ukaahidi kufanya "kila lipaswalo " kumuunga mkono Bwana Maduro.

Mzozo huu ulianzia wapi ?


Rais wa Urusi Vladimir Putin (Kulia) na mwenzake wa Venezuelan Nicolas Maduro ni washirika wa karibu

Bwana Maduro alipata ushindi kwa kura chache katika uchaguzi wa Aprili 2013 baada ya kifo cha aliyekuwa mshirika wake rais Hugo ChƔvez.

Alichaguliwa kwa muhula wa pili Mei 2018 katika uchaguzi ambao ulikosolewa sana na wakaguzi wa kimataifa.

Venezuela imekumbwa na mporomoko wa uchumi , huku uhaba wa chakula na mfumuko wa bei ukiongezeka na ukifikia walau kiwango cha 800,000% mwaka jana.


Bwana GuaidĆ³ amemtuhuma rais Maduro kuwa mtu asiyefaa kuwa rais, na alipata uungaji mkono wa wengi nchini humo pamoja na viongozi wa Marekani na Muungano wa Ulaya .

Serikali ya Maduro inaendelea kutengwa huku nchi nyingi zikiilaumu kwa mzozo wa kiuchumi, ambao umewafanya raia zaidi ya milioni tatu kuihama Venezuela.

Wakati huohuo, serikali ya Moscow imepanua ushirikiano na serikali ya Caracas katika miaka ya hivi karibuni - ikiongeza mauzo ya silahana kuongeza zaidi mikopo kwa nchi hiyo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...