Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 20, 2017

Korea Kaskazini yarusha makombora 3 baharini

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha AFP PHOTO/KCNA VIA KNS Image caption Kombora la Korea Kaskazini Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa mafupi , jeshi la Marekani limesema. Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo moja katika mkoa wa kaskazini wa Gangwon na kuruka kwa umbali wa kilomita 250 kulingana na maafisa wa Korea Kusini. Tangu ifanyie majaribio kombora lake la masafa marefu mwezi uliopita, Pyongyang imetishia kurusha makombora yake katika kisiwa cha Marekani cha Guam. Lakini jaribio hili la hivi karibuni linajiri kufuatia zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini. Maelfu ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini wanaendelea kufanya zoezi la pamoja ambalo hufanywa kwa kutumia Komyupta. Korea Kaskazini: Marekani iliwapora wanadiplomasia wetu Korea Kaskazini: Tutaishambulia Marekani kwa nyuklia Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini Korea Kaskazini yaonywa na Marekani Marekani awali ilikuwa imeripoti kwamba makombora mawili yal...

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.08.2017

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kwa pauni milioni 35 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Alhamisi ijayo. (Daily Telegraph) Chelsea wananajaribu kufanikisha usajili wa pauni milioni 15 wa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, ambaye alicheza chini ya Antonio Conte, Juventus. (Daily Telegraph) Juventus wamewasiliana na Chelsea kumuulizia beki wa kati Gary Cahill. (Sun) Manchester City wamekata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 150. (Sun) Manchester City watapanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 25 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (Times) Mchezaji wa Monaco Thomas Lemar amesema angependa zaidi kujiunga na Manchester United badala ya Arsenal. (Duncan Castles) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Gary Cahill alijiunga na Chelsea mwaka 2012 akitokea Bolt...

Mkuu wa Samsung Lee Jae-yong afungwa jela miaka mitano juu ya rushwa

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Mahakama nchini Korea Kusini imemhukumu bilionea anayetarajiwa kurithi kampuni Samsung Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya utoaji rushwa. Bw Lee alikuwa ameshtakiwa kuhusika katika rushwa katika kashfa ambayo pia ilichangia kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Korea Kusini. Kesi hiyo ilikuwa imevutia sana umma huku hasira zikiendelea kupanda dhidi ya kampuni kubwa za kibiashara za Korea Kaskazini, maarufu kama chaebols. Bw Lee, ambaye amekanusha mashtaka yote, alikuwa amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela hadi miaka 12. Bw Lee, ambaye pia hufahamika kama Jay Y Lee na amekuwa ndiye kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuunda simu duniani, amekuwa kizuizini tangu Februari akikabiliwa na tuhuma kadha za rushwa. Miongoni mwa makosa aliyokabiliwa nayo ni utoaji rushwa, wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi. Lee, 49, pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani wa won 41bn ($36m; £29m) k...

Mwanamke ajishindia $758m kwenye jackpot Marekani

MTEULE THE BEST L Mshirikishe mwenzako Mshindi wa pesa nyingi zaidi kuwahi kujishindiwa na mtu binafsi katika shindano la bahati nasibu Amerika Kaskazini - jumla ya $758.7m (£590m) - amejitokeza kuchukua zawadi yake, na ni mwanamke. Mavis Wanczyk, 53, mama wa watoto wawili, alinunua tiketi yake ya ushindi katika kituo cha mafuta Chicopee, Massachusetts. Mshindi huyo, ambaye namba zake za bahati zilikuwa 6, 7, 16, 23 na 26, na 4 - ameambia wanahabari kwamba tayari ameacha kazi. Zawadi ya juu zaidi ya jackpot katika shindano la bahati nasibu ya kampuni ya US Powerball kuwahi kutolewa ilikuwa $1.6bn, lakini ilienda kwa washindi watatu ambao waligawana pesa hizo Januari 2016. Wasimamizi wa mashindano ya bahati nasibu jimbo la Massachusetts waliambia wanahabari kwamba tiketi ya mwanamke huyo ambayo ilishinda Jumatano imethibitishwa kuwa halisi. "jambo ninalotaka kufanya kwa sasa ni kuketi na ktuulia," alisema Bi lWanczyk. Haki miliki ya picha WBZ-TV) Image capti...

Magazeti ya Tanzania leo August 25 2017 yakiwa na habari zote kubwa kwenye kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya UDAKU, MICHEZO na HARDNEWS.

MTEULE THE BEST Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 25  2017  yakiwa na habari zote kubwa kwenye kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya  UDAKU ,  MICHEZO  na  HARDNEWS .

Yingluck: Mahakama yatoa kibali waziri mkuu wa zamani Thailand akamatwe

MTEULE THE BEST Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Twitter   Mshirikishe mw Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mamia ya wafuasi wa Bi Yingluck walifika nje ya majengo ya mahakama ya juu Bangkok Mahakama ya Juu nchini Thailand imeahirisha kikao cha kutoa hukumu katika kesi ambapo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra ameshtakiwa makosa ya uhalifu ya kuzembea kazini. Majaji hao wakiwa mjini Bangkok wametoa kibali cha kukamatwa kwake wakisema hawaamini alivyosema kwamba amekosa kufika mahakamani kwa sababu anaugua. Mahakama imeahidi kutoa huku tarehe 27 Septemba. Ijumaa, mawakili wa Bi Yingluck waliomba hukumu icheleweshwe na kuambia mahakama kwamba anaugua ugonjwa wa vertigo na hawangeweza kufika kortini. Lakini taarifa rasmi ya Mahakama ya Juu imesema waendesha mashtaka "hawaamini mshtakiwa ni mgonjwa kwani hakuna cheti chochote cha matibabu kilichowasilishwa kwa mahakama, na kwamba hali yake ya afya si mbaya mno...