MTEULE THE BEST
Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa mafupi , jeshi la Marekani limesema.
Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo moja katika mkoa wa kaskazini wa Gangwon na kuruka kwa umbali wa kilomita 250 kulingana na maafisa wa Korea Kusini.
Tangu ifanyie majaribio kombora lake la masafa marefu mwezi uliopita, Pyongyang imetishia kurusha makombora yake katika kisiwa cha Marekani cha Guam.
Lakini jaribio hili la hivi karibuni linajiri kufuatia zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini.
Maelfu ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini wanaendelea kufanya zoezi la pamoja ambalo hufanywa kwa kutumia Komyupta.
- Korea Kaskazini: Marekani iliwapora wanadiplomasia wetu
- Korea Kaskazini: Tutaishambulia Marekani kwa nyuklia
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Korea Kaskazini yaonywa na Marekani
Marekani awali ilikuwa imeripoti kwamba makombora mawili yalikuwa yamefeli , lakini kulingana na tathmini yake mojawapo ya makombora hayo lililipuka wakati huohuo liliporushwa huku mengine mawili yakiruka kwa umbali wa kilomita 250 yakielekea maeneo ya kaskazini mashariki.
Makombora hayo yalirushwa kwa tofauti ya dakika 30 , kulingana na afisa mmoja.
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini ilisema: Jeshi linaangalia kwa umakini hatua ya Korea Kaskazini ya uchokozi.
Maoni