Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Yingluck: Mahakama yatoa kibali waziri mkuu wa zamani Thailand akamatwe

MTEULE THE BEST
Bangkok, Thailand, 25 August 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMamia ya wafuasi wa Bi Yingluck walifika nje ya majengo ya mahakama ya juu Bangkok
Mahakama ya Juu nchini Thailand imeahirisha kikao cha kutoa hukumu katika kesi ambapo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra ameshtakiwa makosa ya uhalifu ya kuzembea kazini.
Majaji hao wakiwa mjini Bangkok wametoa kibali cha kukamatwa kwake wakisema hawaamini alivyosema kwamba amekosa kufika mahakamani kwa sababu anaugua.
Mahakama imeahidi kutoa huku tarehe 27 Septemba.
Ijumaa, mawakili wa Bi Yingluck waliomba hukumu icheleweshwe na kuambia mahakama kwamba anaugua ugonjwa wa vertigo na hawangeweza kufika kortini.
Lakini taarifa rasmi ya Mahakama ya Juu imesema waendesha mashtaka "hawaamini mshtakiwa ni mgonjwa kwani hakuna cheti chochote cha matibabu kilichowasilishwa kwa mahakama, na kwamba hali yake ya afya si mbaya mno kiasi kwamba hawezi kufika kortini."
Mahakama imesema itatoa kibali cha kukamatwa kwake kwani anaweza kuikimbia nchi hiyo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Kadhalika, mahakama imetwaa dhamana ya $900,000 (£703,000) ambayo alikuwa ameiweka wakati wa kuanza kwa kesi hiyo.
Bi Yingluck, amekanusha makosa ya kuzembea kazini yanayohusiana na mradi wa mpunga wa gharama ya mabilioni ya dola.
Iwapo atapatikana na hatia, anaweza akafungwa jela na pia kupigwa marufuku kutoshiriki siasa maishani yake yote.
Bi Yingluck, ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Thailand mwaka 2011, aliondolewa madarakani mwaka 2015.
Kesi dhidi yake iliwasilishwa na serikali inayoungwa mkono na jeshi ambayo ilimuondoa mamlakani.
Lakini bado ni maarufu na anaungwa mkono sana.
Mamia ya wafuasi wake walikusanyika nje ya Mahakama ya Juu mjini Bangkok kabla ya kusomwa kwa hukumu dhidi yake, huku polisi wengi wakishika doria nje ya mahakama hiyo.
Mpango wa Bi Yingluck wa kulipia sehemu ya gharama ya mpunga ulikuwa sehemu ya ahadi zake kuu kwenye kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa, na aliuzindua mwaka 2011 muda mfupi baada yake kuingia madarakani.
Yingluck Shinawatra Bangkok, Thailand, 1 August 2017.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMradi huo wa mpunga ulikumbwa na utata wakati wa utawala wa Bi Yingluck
Lengo la mpango huo lilikuwa kuimarisha mapato ya wakulima na kusaidia kupunguza umaskini mashinani.
Chini ya mpango huo, serikali iliwalipa wakulima karibu maradufu ya bei ya mpunga sokoni kwa mazao yao.
Lakini uliathiri sana uuzaji wa mpunga kutoka Thailand nje ya nchi na kusababishia taifa hilo hasara ya zaidi ya $8bn (£6.25bn).
Serikali pia ilibaki na shehena kubwa ya mpunga ambao haingeweza kuuuza.
Ingawa mpango huo ulikuwa maarufu sana kwa wafuasi wake mashinani, wapinzani waliupinga wakisema ulikuwa ghali sana na ulitoa fursa ya kutokea kwa ulaji rushwa.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yake, Bi Yingluck alisema kwamba hakuhusika katika shughuli za kila siku za kuusimamia mradi huo.
Amesisitiza kwamba yeye ni mwathiriwa wa mateso ya kisiasa.

Yingluck na utata kuhusu mradi wa mpunga
Mei 2011- Yingluck Shinawatra achaguliwa Waziri Mkuu, na muda mfupi baadaye anaanzisha mpango wa kufadhili kilimo cha mpunga
Januari 2014 - Maafisa wa kupambana na rushwa Thailand wamchunguza Bi Yingluck kuhusiana na mradi huo
Mei 2014 - Ashurutishwa kung'atuka baada ya mahakama ya kikatiba kumpata na hatia ya kutumia vibaya mamlaka katika kesi nyingine. Wiki chache baadake, jeshi lawaondoa maafisa wengine waliokuwa wake serikalini.
Januari 2015 - Bunge linaloungwa na jeshi lapitisha sheria ya kumuondoa Bi Yingluck madarakani kwa makosa ya ulaji rushwa kuhusiana na mradi huo wa mpunga, hatua inayompiga marufuku kutoshiriki siasa kwa miaka mitano. Aidha, anafunguliwa kesi.
Agosti 2017 - Bi Yingluck akosa kufika mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu akisema anaugua.

Uongozi wa Bi Yingluck uligubikwa na utata pamoja na upinzani uliokuwa na nguvu.
Yeye ni dada mdogo wa tajiri na waziri mkuu wa zamani wa Thaksin Shinawatrwa na alikuwa akitazamwa na wapinzani wake kama kikaragosi wa kakake ambaye aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2006.
Lakini wawili hao bado ni maarufu sana miongoni mwa maskini mashinani, ingawa wanashukiwa sana na wakazi wa miji na watu wa mapato ya wastani.
Chama chao cha Pheu Thai kimekuwa kikishinda uchaguzi tangu 2001

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...