Rais Dkt. John Magufuli amezungumzia kitendo cha Mbunge wa Monduli (CCM), Julius Kalanga kumuomba apeleke maji jimboni kwake ilihali jimbo hilo limewahi kuongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye pia amewahi kuwa waziri wa maji. Rais Dkt. Magufuli akiwa na Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Akizungumza na wananchi wa Arumeru, ambapo amezindua na kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 jijini Arusha, Rais Magufuli amesema kuwa anampongeza Kalanga kwa kuhamia CCM akitokea CHADEMA kwakile alichosema ni kitendo cha kijasiri. " Kalanga, Mbunge wa Monduli aliwahi kuniomba maji akiwa CHADEMA, lakini amesahau kuwa Lowassa amewahi kuwa Waziri wa Maji, simsemi mzee wangu namaanisha kuwa uzalendo unaanzia nyumbani, nikupongeze Kalanga kwa ujasiri wako wa kurudi huku, maji utapata ", amesema Rais Magufuli Katika hatua nyingine amewaomba Watanzania kumuombea ili awatumikie vyema, " Muendelee kuniombea ili cheo changu cha Urai...