Waandamanaji wapambana na polisi nje ya ubalozi wa Marekani Lebanon Waandamanaji wamepambana na vikosi vya ulinzi nchini Lebanon karibu na ubalozi wa Marekani Kaskazini mwa mji mkuu Beirut. Vikosi vya usalama vimerusha gesi ya kutoa machozi na maji kuwarudisha nyuma waandamanaji wanaopinga hatua ya Trump ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Vikosi vya usalama vilirusha vitoa machozi na maji kuwarudisha nyuma waandamanaji hao waliokuw na bendera. Nao muungano wa nchi za kiarabu umelaanbi hatua hiyo ya Marekani. Kwa nini mji wa Jerusalem ni mtakatifu? Trump: Jerusalem ni mji mkuu wa Israel Wapalestina wampinga Trump kuhusu Jerusalem Mzozo wa Jerusalem: Watu 30 wajeruhiwa Palestina Ulisema kuwa sasa Marekani haiwezi kutegemewa kuwa mpatanishi kwenye amani ya mashariki ya kati. Waandamanaji hao waliokaribia ubalozi wa Marekani walirusha mawe na kuwasha moto barabarani. Vikosi vya usalama vilifunga barabara kuu inayoingia kwenye majengo makuu ya uba...