MTEULE THE BEST Trump aliomba radhi Jumamosi (08.10.2016) kwa kutumia lugha hiyo chafu kuhusu kuwatomasa na kuwabusu wanawake katika mkanda wa video wa mwaka 2005.Kutolewa kwa mkanda huo kumeitibuwa kampeni yake na kusababisha kulaaniwa na wanachama wenzake kutoka chama chake mwenyewe cha kisiasa. Trump amesema katika taarifa ya video iliowekwa kwenye mtandao wa Twitter "Nimefanya mambo ninayoyajutia.Mtu yoyote anayenifahamu anajuwa kwamba maneno haya hayamaanishi mim ni mtu wa aina gani. Nimesema nilikuwa sio sahihi na naomba radhi." Wanachama wenzake wa chama cha Republikan wamelaani lugha aliyoitumia mgombea huyo.Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan afisa mwandamizi wa chama hicho amesema "amechafuliwa " na matamshi hayo na amefuta tukio la kampeni lililokuwa lifanyike Wisconsin pamoja na Trump hapo Jumamosi. Wanachama wenzake wamuacha mkono Spika wa Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani Paul Ryan. Reince Preibus mwenyekiti wa Kam...