MTEULE THE BEST
Siku mbili baada ya kuipiga nchi ya Haiti, kimbunga Hurricane Matthew kimeendelea kusababisha madhara makubwa hususan maeneo ya Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.
Idadi ya watu waliokufa imefikia 100 wengi wakiwa ni kutoka mji wa Roche-Ć -Bateau na Jeremie.
Nyumba nyingi zimeharibika vibaya, huku wakaazi wake wakiachwa bila chakula na maji.
Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa asilimia 80 katika baadhi ya maeneo zimehariwa vibaya, miti imengooka na mazao yamezolewa na maji.
Maoni