Sekta ya kilimo iliimarika kwa sehemu kubwa ikishinikizwa na uwekezaji wa miundo msingi na uzalishaji wa vyakula. Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema 2018 ndio mwaka utakaoshuhudia ukuwaji mkubwa wa kiuchumi duniani tangu 2011. Hatahiyo uwezekano wa ukuwaji huo kwa mataifa yanayoendelea kusini mwa jangwa la Sahara hautokuwa rahisi katika miaka mitano ijayo. Je ni kwanini? IMF linakadiria kwamba ukuwaji wa pato jumla la nchi katika mataifa yaliopo kusini mwa jangwa la Sahara utaongezeka taratibu kati ya 2018 na 2019 kwa asilimia 3.4% hadi 3.7%, mtawalaia, huku bei za bidhaa zikipanda. Shirika hilo linalotoa mikopo kwa mataifa duniani hatahivyo linasema lina matumaini kuhusu uwezekano huo wa ukuwaji wa uchumi likitabiria ukuwaji wa hadi 3.9% mwaka huu kutoka 3.8% mwaka 2017 . Ukuwaji wa uchumi katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sagara umekuwa kwa asilimia 2.4 baada ya kushuka kwa 1.3 mnamo 2016 Limeonya hatahivyo kwamba kasi hiyo huenda isiwe ya muda mr...