Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais akutana na Mabalozi wa Palestina na Japan Ikulu

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amekutana na Balozi wa Palestina pamoja na Balozi wa Japan jijini Dar es salaam.    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam

Mama Samia aionya Takukuru kukumbatia wala rushwa

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameionya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Rombo kutokana na taarifa kwamba baadhi ya maofisa wake wanatumika kuwalinda watendaji wa serikali wanaojihusisha na rushwa.  Samia alitoa onyo hilo jana akiwa katika sehemu ya ziara yake ya siku tano ya kikazi mkoani Kilimanjaro.  Alisema asilimia 90 ya watendaji wa serikali katika wilaya hiyo wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakutoa huduma kwa wananchi, huku akiionyooshea kidole taasisi hiyo kwa kuwafumbia macho watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rombo.  "Nasikitika kusema kuwa asilimia 90 ya watendaji wa halmashauri wanafanya kazi kwa kupokea rushwa ili kuwaudumia wananchi. Niwaonye na niwaambie taarifa hizo tunazo na majina yenu tunayo. Jirekebisheni mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.  “Takukuru sidhani kama mnatambua wajibu wenu au nimeona jengo tu ambalo halina utendaji? Wananchi wengi wanashindwa kup...