Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mama Samia aionya Takukuru kukumbatia wala rushwa



Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameionya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Rombo kutokana na taarifa kwamba baadhi ya maofisa wake wanatumika kuwalinda watendaji wa serikali wanaojihusisha na rushwa. 

Samia alitoa onyo hilo jana akiwa katika sehemu ya ziara yake ya siku tano ya kikazi mkoani Kilimanjaro. 

Alisema asilimia 90 ya watendaji wa serikali katika wilaya hiyo wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakutoa huduma kwa wananchi, huku akiionyooshea kidole taasisi hiyo kwa kuwafumbia macho watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rombo. 

"Nasikitika kusema kuwa asilimia 90 ya watendaji wa halmashauri wanafanya kazi kwa kupokea rushwa ili kuwaudumia wananchi. Niwaonye na niwaambie taarifa hizo tunazo na majina yenu tunayo. Jirekebisheni mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa. 

ā€œTakukuru sidhani kama mnatambua wajibu wenu au nimeona jengo tu ambalo halina utendaji? Wananchi wengi wanashindwa kupata huduma na wanapiga simu kwenye ngazi za juu ili kuomba msaada na wanakiri kutoa pesa ili kutekelezewa jambo lao. Haipendezi na hii ni dhambi kubwa sana, jirekebisheni isiwe tu tuna taasisi jina," alisema. 

Aliitaka taasisi hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na kujitahidi kutunza siri kwa wananchi wote zinazotoa taarifa na kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwa watakaobainika kujihusisha na rushwa. 

ā€œSisi tumewaweka hapo ili msaidie wananchi kupata haki zao kwa wakati na baadaye wapate nguvu ya kwenda kwenye majukumu yao na kuzalisha na badala yake mmekuwa chanzo cha chuki na ukandamizaji wa haki za wananchi, hatutakubali na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yenu,ā€ alisema Samia. 

Pia alisema katika halmashauri hiyo, suala la rushwa ya ngono kwa watendaji wa kiume na ubaguzi wakati wa uwajibikaji, limekuwa likishika kasi siku hadi siku. 

Kuhusu uhusiano kati ya halmashauri hiyo na wananachi, Makamu wa Rais aliwataka viongozi na watendaji wa kuacha malumbano na badala yake washirikiane katika kuwahudumia wananchi 

Alisema malumbano yanayotokana na itikadi za vyama vya siasa yanawacheleweshea wananchi maendeleo na kupoteza ari ya kuwajibika miongoni mwa watendaji wa ngazi ya chini. 

ā€œHata kama umepewa kazi na mjomba wako, ukifika hakikisha unawajibika na kuwatumikia wananchi na si kuanzisha malumano na misuguano isiyo na tija. Hatutakuvumilia unapokwamisha maendeleo hayo,ā€ alisema Samia. 

ā€œMkishindwa kushirikiana maendeleo yatarudi nyuma na watakaoathirika si Rais (John Magufuli wala mimi bali ni wananchi ambao siku zote  wanatulalamikia kuhusu utendaji usio wa kuridhisha kutokana na kutokuelewana kwa baadhi ya viongoziā€, aliongeza. 

Akisoma taarifa ya wilaya, Mkuu wa Wilaya hiyo, Agnes Hokororo, alisema ziko  changamoto nyingi wanazokabilina nazo lakini kubwa zaidi ni maji hasa ukanda wa chini 

ā€œTunaiomba serikali kuu kutufikiria namna ya kutusaidia wananchi wa ukanda wa chini wapate maji safi na salama kwa kipindi cha mwaka mzima,ā€ alisema

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...