Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAJANGA

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Idai yaongezeka kwa kasi nchini Msumbiji

Wafanyakazi wa shirika la uokoaji wakiwa wanajiandaa kuondoa miili kutoka kwenye helikopter Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na kimbunga Idai kilichoikumba eneo la kusini mwa Afrika zaidi ya juma moja lililopita,imeongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi. Idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 242 mpaka 417,waziri wa ardhi na mazingira nchini humo Celso Correia ameeleza. Idadi hii mpya inafanya waliopoteza maisha Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kufikia 700. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi. Kimbunga kimeua takribani watu 259 nchini Zimbabwe na Malawi 56.Watu walipoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko. Lakini Umoja wa mataifa limesema maafisa wataweza kutathimini madhara pale maji yatakapopungua. Maelfu ya watu wakiwa wanasubiri kuokolewa kutoka kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kusini mwa Afrika Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinaadamu, OCHA imesema kuwa mto wa Buzi na ...