mteulethebest Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wang Yi na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan, Jumatano na Alhamisi mjini Vienna, wamefanya majadiliano ya dhati, ya kina, ya kuangalia mazingira halisi na ya kiujenzi kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Viongozi hao walijadiliana juu ya kuondoa mambo yanayokwamisha uhusiano kati ya China na Marekani na kuzuia uhusiano huo usizorote. Wang alifafanua kwa ukamilifu msimamo mzito wa China kuhusu suala la Taiwan. Pia walibadilishana maoni kuhusu hali ya eneo la Asia na Pasifiki, Ukraine na masuala mengine ya kimataifa na kikanda wanayofuatilia kwa pamoja, na kukubaliana kuendelea kutumia vyema njia hii ya kimkakati ya mawasiliano.