Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NDEGE ZA KIVITA

Marekani yatuma ndege zaidi za kivita katika Mashariki ya Kati

    Ndege ya kivita ya F-22 Raptor inaonekana ikiruka baada ya kujaza mafuta kwenye pwani ya mashariki ya Marekani. © Pentagon / Mwalimu Sgt. Jeremy Lock Maafisa wa Marekani wametangaza kutumwa kwa ndege za F-22, wakitaja operesheni za anga za Urusi "za uchochezi". Marekani yatuma ndege zaidi za kivita katika Mashariki ya Kati Jeshi la Marekani limetuma ndege za ziada za kivita katika Mashariki ya Kati baada ya kuishutumu Urusi kwa shughuli za ndege "zisizo salama" katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na wakati wa matukio kadhaa nchini Syria. F-22 Raptors pamoja na Kikosi cha 94 cha Wapiganaji wametumwa kutoka Kambi ya Jeshi la Anga la Langley huko Virginia, kulingana na Kamandi Kuu (CENTCOM), ambayo inasimamia operesheni za kijeshi za Amerika Mashariki ya Kati, Asia ya Kati na sehemu za Afrika. Uamuzi huo ulikuwa sehemu ya "maonyesho mengi ya usaidizi na uwezo wa Marekani kutokana na tabia mbaya na zisizo za kitaalamu za ndege za Kirusi," CENTCOM ilisema k...

Uingereza yazindua ndege mpya zisizo na rubani kwa Ukraine

© Wizara ya Ulinzi ya Uingereza  Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imeonyesha ndege za kisasa zisizo na rubani zinazotarajiwa kutumwa kwa Ukraine ndani ya wiki kadhaa kama sehemu ya kampeni ya London ya kuipatia Kiev silaha za masafa marefu. Siku ya Jumatano, wizara ilitoa video kwenye Twitter iliyo na aina kadhaa za ndege zisizo na rubani. Mmoja alionekana akiangusha torpedo juu ya maji, huku mwingine akionyeshwa akiruka kutoka nchi kavu huku akiongozwa na opereta, na wa tatu alitolewa kwenye sitaha ya meli ya wanamaji. "Uwezo muhimu sasa uko kwenye mkataba," video hiyo inasema. "Usafirishaji wa kwanza utawasili mwezi ujao." Wizara ilisema kwamba UAVs zitatolewa kwa Ukraine kama sehemu ya kifurushi cha msaada cha pauni milioni 92 (dola milioni 116) kilichotangazwa mapema wiki hii. Msaada huo unatarajiwa kununuliwa kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Ukraine, utaratibu wa kutoa msaada wa haraka wa kijeshi kwa Kiev unaojumuisha Uingereza, Norway, Uholanzi, Denmark, Sweden, Ice...

RAIS APINGANA NA UAMUZI WA BUNGE

Trump akaidi uamuzi wa bunge na kuamua kuiuzuia silaha Saudi Arabia zenye thamani ya $8bn Rais Trump, akiwa pamoja na mwanamfalme wa Saudia wanashika chati inayoonyesha mauzo ya silaha kwa Saudia Rais huyo wa Marekani ametumia kura ya turufu kufutilia mbali uamuzi wa bunge la Congress la kuzuia mauzo ya silaha yenye thamani ya $8bn kwa Saudia na UAE. Donald Trump alisema kuwa maamuzi hayo matatu yatadhoofisha uwezo wa Marekani ulimwenguni na kuharibu uhusiano wake na washirika wake . Hatua hiyo inajiri baada ya mabunge yote mawili kupiga kura ya kuzuia mauzo hayo. Baadhi ya wabunge wanasema kwamba walihofia kwamba silaha hizo huenda zikatumiwa dhidi ya raia katika mgogoro wa Yemen. Wameshutumu vitendo vya Saudia nchini Yemen pamoja na mauaji ya mwaka jana ya mwandishi Jamal Khashoggi. Hatahivyo bunge le seneti litapiga kura baada ya siku moja ili kuona iwapo litakaidi uamuzi wa bwana Trump , kulingana na kiongozi wa wengi katika chama cha Republican Mitch Connel. Lakin...

RUSSIA NA CHINA ZAFANYA DORIA YA PAMOJA MAREKANI YALIA

Doria ya pamoja ya Urusi - China yazua tumbo joto Japan na Korea Kusini Korea Kusini ilisema kuwa ndege ya kijeshi ya Urusi aina ya A-50 ilikiuka anga yake mara mbili Urusi inasema kuwa imetekeleza doria yake ya kwanza ya pamoja na China , hatua iliyozifanya Korea Kusini na Japan kutuma ndege za kivita angani. Waziri wa ulinzi nchini Urusi amesema kuwa ndege nne aina ya bombers zikisaidiana na zile za kivita zilipiga doria katika njia ambayo hazikupangiwa kupitia katika maji ya Japan na bahari iliopo mashariki mwa China. Korea Kusini inasema kuwa ndege zake zilirusha makombora ya kutoa onyo wakati ndege za kijeshi za Urusi zilipoingia katika anga yake. Japan imelalamika kwa Urusi na Korea Kusini kwa tukio hilo. Kisa hicho kilitokea juu ya visiwa vinavyozozaniwa vya Dokdo/Takeshima ambavyo vinamilikiwa na Korea Kusini lakini Japan pia inadai kuwa vyake. Korea Kusini inasema kuwa ndege za kijeshi za Urusi na China ziliingia katika anga yake ilio na ulinzi mkali ya KADIZ ...

MAREKANI YALIPIZA KISASI KWA IRAN

Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho. Iran haijasema chochote kuhusu hilo. Mwezi Juni, Iran iliangusha ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha hofu ya kutokea mzozo wa kijeshi. Awali Tehran ilisema imekamata ''meli ya kigeni'' na wafanyakazi wake 12 siku ya Jumapili kwa kusafirisha mafuta kinyume cha sheria. Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kwa kushambulia meli zake tangu mwezi Mei.Tehran ilikana shutuma hizo. Raisi Donald  Trump  amesemaje ? Akizungumza Ikulu, Trump amesema ''Ninataka kuwajulisha kuhusu tukio lililotokea kwenye eneo la mpaka wa Hormuz leo lililohusisha meli yetu ya kijeshi. Chombo hicho kilichukua hatua ya kujilinda dhidi ya nde...

Uturuki imepokea shehena ya kwanza ya makombora ya Kirusi ya S-400 licha ya upinzani mkali kutoka Marekani

Makombora ya Kirusi yawasili Uturuki licha ya vikwazo vya Marekani Makombora ya S-400 ni moja ya zana hatari zaidi za kutungua ndege angani Uturuki imepokea shehena ya kwanza ya makombora ya Kirusi ya S-400 licha ya upinzani mkali kutoka Marekani . Shehena hiyo imepokelewa katika uwanja wa ndege wa jeshi leo Ijumaa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara. Hatua hiyo ya Uturuki kwa hakika itaikasirisha Marekani ambayo tarayi imeshaonya kuwa nchi hiyo haiwezi kumiliki zana za kijeshi za Urusi na Marekani kwa pamoja. Makombora ya S-400 kutoka Urusi ni ya kujilinda na ndege vita, na wakati hu huo Uturuki imewekeza vilivyo katika ununuzi wa ndege vita aina ya F-35 kutoka Marekani. Mzozo unatoka wapi ? Uturuki imeshasaini mkataba wa kununua ndege vita 100 aina ya F-35 kutoka Marekani. Pia kampuni za Kituruki zinatengeneza takribani vipuri 937 vya aina hiyo ya ndege. Uturuki na Marekani zote ni nchi wananchama wa Umoja wa Kujihami wa Nato, ambapo Urusi yaonekana ni adui mkuu ...