Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ITALY

SIMIYU YAJIPANGA KUPAMBANA NA COVID-19

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  mkoa umetenga shule za Sekondari za Bweni za Serikali kuwa maeneo ambayo yatatumika kuwahifadhi washukiwa wa Virusi vya Corona  endapo watapatikana mkoani hapa;  baada ya serikali  kufunga shule na vyuo nchini kwa siku 30 lengo likiwa kukabiliana na ugonjwa huo. Mhe. Mtaka ameyasema hayo wakati akipokea mchango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya  shule ya sekondari Anthony Mtaka uliotolewa na umoja wa madhehebu ya kikirsto Lamadi na kuongeza kuwa mbali na maeneo ya shule Mkoa pia umetenga maeneo ya hoteli ambayo yatatumika endapo washukiwa/watu wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huo ambao hawatahitaji kukaa kwenye maeneo ya shule. "mkoa hautatumia hoteli kwa ajili ya kuhifadhi mtu yeyote atakayeshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona badala yake tutatumia shule za zetu za sekondari za bweni lakini ikitokea mtu anahitaji kukaa hotelini tayari tumeandaa hoteli za kutosha"alisema Mtaka. " ...

CORONA| EPL, LIGUE 1, BUNDESLIGA, LALIGA, UEFA, UUROPA , ITALY, N.K ZASIMAMISHWA

Coronavirus : Mechi za Ligi ya soka ya England kuahirishwa hadi tarehe 3 Aprili Mechi za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi tarehe 3 Aprili kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona. Mashindano yote Ligi ya soka ya Ulaya, mkiwemo Championi Ligi na Ligi ya Ulaya, mechi ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus. Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa. Katika Championi Ligi, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa. Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa. Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa. Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatol...

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 17.11.2019:

Gareth Bale Manchester United wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale,30, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Sun on Sunday) Paris St-Germain wanawezekana kuwa kikwazo kikubwa kwa mpango wa Manchester United wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19 mwenye thamani ya pauni milioni 120. (Sunday Express) PSG pia wanamtaka kiungo wa Liverpool Adam Lallana,31.(Sunday Mirror) Manchester United wanamtazama kwa karibu winga wa West Bromwich Albion Matheus Preira, anayecheza kwa mkopo akitokea Sporting Lisbon. (Mirror) Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho Arsenal wanajiandaa kumuwania mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uturuki, ambaye anaweza kuuzwa na Juventus kama ofa ya kuridhisha itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.(Tuttosport - in Italian) Barcelona wanajadili mkataba mpya na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32. (Mundo Deportivo - in Spanish) Mshambuli...