VIBAKA WAVUNJA MAKAZI YA KADINALI ERNEST SIMONI (97) FLORENCE
Florence, Italia Tukio la kusikitisha limetokea katika Curia ya Piazza Duomo, Florence. Makazi ya Muadhama Kadinali Ernest Simoni, (97), ambaye ni MAlbania na shahidi haiwa mateso ya Kanisa chini ya utawala wa Kikomunisti wa Enver Hoxha, yamevamiwa na wezi sugu. Yaliyotokea Kwa mujibu wa gazeti la Corriere Fiorentino na shirika la habari la Adnkronos, tukio limetokea mchana wakati hakuna mtu nyumbani. Kadinali Simoni yupo London kwa mwaliko wa kukutana na Mfalme Charles III wa Uingereza, huku mpwa wake Tonin Simoni na mkewe wakiwa mgahawani kwao Borgo Albizi. Wezi walifanya kazi kwa utulivu wa kutisha. Walivunja mlango wa kinga na kubomoa sehemu ya ukuta kwa kutumia patasi nzito (scalpelli) kisha wakafungua makabati na masanduku. Waliondoka na kiasi cha takriban €30,000, vito vya dhahabu, na hata kadi ya ukaazi ya Kadinali. Mpwa wake amesema: "Tumeshtushwa sana. Tulijihisi salama. Hatukutegemea kabisa wizi wa kinyama kama huu katikati ya Piazza Duomo. Hii ni aibu kwa jiji." I...