Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TOTTENHAM

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, ambaye aliondoka Anfield kwa kima cha £142m mwaka 2018. (ESPN) Paris St-Germain imekubali kulipa £28m kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, 29, kutoka Everton. (Mail) Toffees wanaendelea kushauriana na Crystal Palace kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, kwa pauni £80m. (Sky Sports) Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa £80m. (Evening Standard) Paul Dybala Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen, 27, wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark amesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70. (Mail) United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory ...