Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SAYANSI

Je ni mataifa gani yanayoruhusu kujitoa uhai kwa hiari?

David Goodall anasema anataka kufa kwa heshima Mwanasayansi mwenye umri wa miaka 104 David Goodall ameaga nyumbani Australia kuanza safari ya kimataifa kwenda kujitoa uhai. Sio kwamba mwanaekoljia huyo anaugua mahututi, La, anatamanai kuharakisha kifo chake. Sababu kuu ya uamuzi wake anasema ni kupungua kwa uhuru wake. "Najuta kufika umri huu," Dkt Goodall alisema mwezi uliopita katika sherehe ya kuzaliwa kwake, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Australia. "Sina raha. Nataka kufa. Sio jambo la kuhuzunisha, kinachohuzunisha ni kwamba mtu anazuiwa kufa." Ni jimbo moja pekee Australia lililohalalisha kujitoa uhai mwaka jana kufuatia mjadala mkali uliozusha mgawanyiko, lakini ili mtu kuruhusiwa, ni sharti awe anaugua mahututi. Dkt Goodall anasema atasafiri kwenda katika kliniki moja nchini Uswisi kujitoa uhai kwa hiari. hatahivyo anasema anachukizwana kwamba anaondoka nyumbani ili aweze kufanya hivyo. Carol O'Neill anaandamana ...