Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 23, 2017

Mahakama yamzuia waziri mkuu wa Pakistan kushika wadhifa wa serikali

MTEULE THE BEST Pakistan's Supreme Court has recommended an anti-corruption case against Mr Sharif Mahakama kuu nchini Pakistan imemzuia waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif, kutokana na kushika wadhifa wowote serikalini kufuatia uchunguzi kwa madai ya ufisadi. Uamuzi huo unakuja baada ya uchunguzi kuhusu utajiri wa familia yake na ufichuzi wa mwaka 2015 wa Panama Papers, uliowahusisha watoto wake na akaunti za benki ugenini. Bwana Sharif mara kwa mara amekana kufanya lolote baya. Amri hiyo ilitolewa na jopo la majaji watano. Mahakama ilifurika siku ya Ijumaa na usalama zaidi ukawekwa kwenye mji mkuu, huku maelfu ya wanajeshi na polisi wakitumwa. Waziri wa mambo ya ndani nchini Pakistan Chaudhry Nisar Ali Khan, alimshauri Bwana Sharif kukubali uamuzi wa leo. Mahakama imependekeza kufanyika kesi za ufisadi dhidi ya watu kadhaa akiwemo Bwana Sharif, mtoto wake wa kike Maryam na mumewe Safdar, waziri wa fedha Ishaq Dar na wengine kadhaa. Hakuna waziri mkuu wa ...

Google kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika

MTEULE THE BEST Google kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika Google ina mipango ya kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika kuhusu njia za kutumia mitandao katika kipindi cha miaka mitano inayokuja kwa lengo la kuwawezesha kupata ajira. Msemaji wa kampuni hiyo anasema kuwa, Google pia itawapa mafunzo wahandisi wa mitandaoi 100,000 nchini Nigeria, Kenya na Afrika Kusini. Mwezi Machi Google ilisema kwa ilikuwa imefikia lengo lake la kuwapa mafunzo watu milioni moja. Mkurugenzi wa Google Sundar Pichai anasema kuwa kampuni hiyo imejitolea kuwandaa watu wengine milioni 10 kwa ajira siku za usoni katika kipindi cha miaka mitano inayokuja. Kulingana na Google blog mafunzo hayo yanayotolewa kwa lugha kadha zikiwemo Kiswahili, Hausa na Zulu, na yatahakikisha kuwa asilimia 40 ya watu ambao watapewa mafunzo hayo ni wanawake

Boko Haram wauwa zaidi ya watu 60, Nigeria

MTEULE THE BEST Zaidi ya watu 40 wauawa wakati wa mapigano na Boko Haram Nigeria Zaidi ya watu 40 wameuawa wakati wa jaribio la kuwaokoa watu waliotekwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram . Takriban watu watano wa kampuni ya kuchimba mafuta waliuawa, kwa mujibu wa chuo cha Maiduguri. Wanajeshi pia waliuawa wakati wa uvamizi huo. Idadi hiyo kubwa ya vifo ni pigo kwa serikali ambayo inasisitiza kuwa kundi la Boko Haram limeshindwa. Takriban watu 20,000 wameuawa na maelfu ya wengine kutekwa tangu Boko Haram ianzishe harakati zake mwaka 2009. Katika kisa kibaya zaidi Boko Haram waliteka wasichana 276 kutoka shule ya wasichana kaskazini mashariki mwa Nigeria ya Chibok mwaka 2014. Tangu wakati huo wamewaachili zaidi ya wasichana 100 kubadilishana na wapiganaji. Taarifa za kina kuhusu kile kilichotokea siku ya Jumanne hazijulikani, huku ripoti za awali kutoka kwa jeshi, zikisema kuwa watu ambao walitekwa waliokuwa ni wakifanya kazia katika chuo cha Maiduguri waliachi...

Bi Mugabe amtaka mumewe kumtangaza ''mrithi'' wake

MTEULE THE BEST Rais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe Rais wa Zimabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi. ''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno alke litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe. Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao. Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.

LIVERPOOL KUWEKA KAMBI UJERUMANI SIKU 8

MTEULE THE BEST Kikosi cha Liverpool tayari kimewasili mjini Munich Ujerumani ambako kitakaa kwa siku nane  nchini humo kikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka ya England. Wakiwa huko, majogoo hao wa jiji chini ya kocha mkuu,  Mjerumani Jurgen Klopp watashiriki kombe dogo la AUDI CUP ambalo litajumuisha wenyeji wao mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich, miamba ya Hispania, Atletico Madrid na Napoli ya Italia. Liverpool itasafiri kwenda Berlin kucheza mechi ya kirafiki Julai 29 mwaka huu dhidi ya Hertha Berlin, kabla ya kurejea Munich kutupa karata ya kwanza katika mashindano ya AUDI CUP ambapo itaanza kibarua kwa kuwavaa Bayern Munich Agosti mosi mwaka huu.

Wapalestina warudi kufanya ibada katika eneo takatifu

MTEULE THE BEST Wanaoabudu walijaa katika eneo la jumba hilo baada ya viongozi wa Kiislamu kuondoa marufuku ya kususia ya wiki mbili kufuatia hatua hiyo ya Israel. Wapalestina wamerudi katika eneo muhimu la kufanya ibada mjini Jerusalem kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wiki mbili baada ya Israel kuondoa vizuizi vya kiusalama. Wanaoabudu walijaa katika eneo la jumba hilo baada ya viongozi wa Kiislamu kuondoa marufuku ya kususia ya wiki mbili kufuatia hatua hiyo ya Israel. Mpango huo uliwekwa na Israel baada ya mauaji ya maafisa wawili wa polisi ya Israel karibu na eneo hilo. Vizuizi vya mwisho viliondolewa siku ya Alhamisi baada ya siku kadhaa za ghasia ambapo watu saba waliuawa. Wapalestina wamepinga kwa nguvu kuwekwa kwa vizuizi hivyo vya kiusalama ,wakidai kuwa ni jaribio la Israel kudhibiti mji huo wa zamani unaojulikana na Waislamu kama Harma al-Sharif huku Wayahudi wakiliita hekalu la mlimani. Makundi ya raia wa Palestina walionekana wakiimba na kucheza den...

Bill Gates apigwa chini kwa utajiri duniani

MTEULE THE BEST Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos amempiku Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos amempiku Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 90.6. Ongezeko la hisa za Amazon siku ya Alhamisi linamaanisha kwamba thamani ya bwana Bezos imeishinda ile ya mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kulingana na jarida la Forbes. Bwana Bezos anamiliki mara tano ya hisa hizo ambazo thamani yake imepita dola bilioni 500. Katika miaka ya hivi karibuni, aliangazia biashara yake ya roketi ya angani ya Blue Origin na gazeti la Washiington Post, ambalo anamiliki. Vifaa vya kiteknolojia vimeongeza ukuwaji wa thamani za biashara kama vile Bezos na Mwanzilishi wa fecebook Mark Zuckerberg. Hivi hapa vitu vitano kuhusu bwana Beezos ambavyo ungefaa kuvijua: -Matumizi yake yanaongezeka. -mapema mwaka huu bwana Bezos alilipa dola milioni 23 kununua eneo la kumbukumbu la kiwanda cha ngu cha zamani mjini ...

Marekani kuziwekea wikwazo Urusi, Iran na Korea Kaskazini

MTEULE THE BEST Baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini. Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiadhibiwa kufuatia majaribio ya makombora. Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili audhinishe na kuwa sheria kamili. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anashutumiwa kwa kuibua silaha hatarishi za nyuklia kila kukicha Akizungumza katika baraza hilo wawakilishi David Ciciline kutoka chama Democratic amesema hatua kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi. Amesema hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita. Naye Ted Poe kutoka chama cha Republican amesisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea kaskazini pia. Rais wa Iran Hassan Rouhani ameahidi kuondoa migogoro ya kimataifa inayoikabili nchi hiy...

Jose Mourinho anasema Manchester United 'inafaa zaidi' kwa ajili ya jitihada za cheo

MTEULE THE BEST Manchester United ni "bora zaidi" ili kushinda Ligi Kuu ya msimu huu lakini lazima iwe "mengi, bora zaidi" kwa changamoto kwa Ligi ya Mabingwa, anasema meneja Jose Mourinho. United alishinda Kombe la Ligi na Europa League na kumaliza sita katika ligi ya msimu wa kwanza wa Mourinho. Alipoulizwa kama alikuwa akielezea cheo cha ndani ya msimu huu, aliiambia BBC Sport: "Tunajiandaa vizuri zaidi kwa hilo." United amesaini Romelu Lukaku na Victor Lindelof hadi sasa msimu huu. "Msimu huu utakuwa vigumu zaidi lakini nadhani tuna hali nzuri ya kupambana na Ligi Kuu," Mourinho aliiambia BBC Sport. "Nadhani msimu huu sisi ni vifaa kidogo bora. Sisi ni dhidi ya timu ya ajabu, dhidi ya uwekezaji wa ajabu. "Lakini naamini katika kundi letu, roho yetu, kwa huruma yetu, katika umoja wetu. Ninawaamini wavulana wangu na tutajaribu." Kama wamiliki wa Ligi ya Europa, United amehitimu moja kwa moja kwa h...

Acacia yakataa kuilipa Tanzania deni la $180b

MTEULE THE BEST Acacia yakataa kuilipa Tanzania deni la $180b Serikali ya Tanzania imesema kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu yenye makao yake nchini Uingereza Acacia inadaiwa na walipa kodi dola bilioni 180  2017-07-25T14:00:51+00:00 Lori linalotumika katika ubebai wa madini Serikali ya Tanzania imesema kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu yenye makao yake nchini Uingereza Acacia inadaiwa na walipa kodi dola bilioni 180 ,kama malipo ya adhabu na riba, kulingana na taarifa ya kampuni hiyo. Takwimu hiyo ni kulingana na ufichuzi uliofanywa na tume mbili za rais kuhusu sekta ya uchimbaji madini. Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Awamy deni hilo linalodaiwa Acacia linasimia mapato yaliopatikana ambayo hayakutajwa kutoka kwa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi katika kipindi cha mwaka 2000 na 2017. Ikijibu, Acacia imepinga madai hayo na kusema kuwa inatafuta njia mbadala Uchunguzi uliofanywa na tume hizo za rais uliishutumu Acacia kwa kufanya operesheni zake k...

RONALD:NEYMAR USIENDE PSG ASEMA AKIWA CHINA

MTEULE THE BEST ₩ € P £ A: Barcelona ni tayari kutoa £ 80m kwa Liverpool na Brazil kiungo Philippe Coutinho, 25. (Jumapili Mirror) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema Coutinho "amefurahia" kwenye klabu baada ya mazungumzo akiwa na mchezaji akiwa na riba ya Barca. (ESPN FC) Barcelona wanaamini kusaini mchezaji wa Coutinho anaweza kumsaidia mwenye umri wa miaka 25 wa timu ya kimataifa ya Neymar, ambaye ameunganishwa na kuhamia Paris St-Germain. (Barua pepe Jumapili) PSG inazidi kujiandikisha mbele ya Neymar kwa £ 196m kutoka Barcelona, ​​na Brazil inadaiwa kuwa imekubali mkataba wenye thamani ya £ 27m kwa mwaka baada ya kodi. (Jumapili Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekataa mbele Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 28, ni karibu na £ 70m kwenda Paris St-Germain. (Standard) Liverpool na Manchester City bado wanapigana na saini ya kusaini Monaco mwenye umri wa miaka 18 mbele Kylian Mbappe. (Le 10 Sport, kupitia Nyota Jumapili) K...

Vurugu zaendelea Jerusalem

MTEULE THE BEST Vurugu zaendelea Jerusalem Wapalestina wawili wameuwawa katika makabiliano na jeshi la Israel hapo jana, wakati jeshi hilo lilipoizingira nyumba ya mshambuliaji baada ya vurugu zilizotokana na hatua kubwa za usalama katika eneo tete takatifu. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wake wa ndani hapo kesho likijikita katika ongezeko la vurugu baada ya Misri, Ufaransa na Sweden kutaka mkutano wa dharura wenye kujadili namna ya kufanikisha jitihada za kudhibiti vurugu za Jerusalem. Vifo hivi vya watu wawili vinatokea baada ya vitendo vya umwagikaji damu siku ya Ijumaa, ambapo kijana wa Kipalestina wa umri wa miaka 19 aliuwauwa walowezi watatu wa Kiisrael katika Ukingo wa Magharibi na Wapalestina watatu kuuliwa na jeshi la Israel. Vurugu hizo vilevile zilitokea mashariki mwa Jerusalem na katika vijiji vingine vya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi, karibu na Jerusalem

UCHUMI WA KOREA KASKAZINI WAPANDA

MTEULE THE BEST Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini uliimarika kwa haraka katika kipindi cha miaka 17 iliopita licha ya kuwekewa vikwazo kutokana na mpango wake wa kinyuklia na utengenezaji wa makombora ya masafa marefu. Uzalishaji wa bidhaa nchini humo ulikuwa kwa asilimia 3.9 2016 ikilinganishwa na mwaka uliopita kulingana na benki ya Korea. Ukuwaji huo unatokana na uchimbaji madini, kawi na uuzaji wa bidhaa nchini China. Marekani imekuwa ikiitaka Beijing kukata biashara na Pyongyang huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu mipango ya kinyuklia ya rais Kim Jong Un. China ndio mshirika pekee mkuu wa Korea Kaskazini na mfadhili mkubwa wa misada nchini humo. Wiki iliopita China ilitoa data ikidai kuwa Korea Kaskazini haina uwezo mkubwa kama inavyodaiwa na rais Trump. Lakini huku Beijing ikisitisha ununuzi wa mkaa kutoka Korea Kaskazini, imeendelea kufanya biashara ya chuma na bidhaa nyengine. Ijapokuwa Korea Kaskazini haichapishi data za kiuchumi , benki kuu ya Korea Kusini in...