Mahakama yamzuia waziri mkuu wa Pakistan kushika wadhifa wa serikali

MTEULE THE BEST

Pakistani Prime Minister Nawaz Sharif arrives in Germany to meet German Chancellor Angela Merkel, 11 November 2014
Pakistan's Supreme Court has recommended an anti-corruption case against Mr Sharif
Mahakama kuu nchini Pakistan imemzuia waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif, kutokana na kushika wadhifa wowote serikalini kufuatia uchunguzi kwa madai ya ufisadi.
Uamuzi huo unakuja baada ya uchunguzi kuhusu utajiri wa familia yake na ufichuzi wa mwaka 2015 wa Panama Papers, uliowahusisha watoto wake na akaunti za benki ugenini.
Bwana Sharif mara kwa mara amekana kufanya lolote baya. Amri hiyo ilitolewa na jopo la majaji watano.
Mahakama ilifurika siku ya Ijumaa na usalama zaidi ukawekwa kwenye mji mkuu, huku maelfu ya wanajeshi na polisi wakitumwa.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Pakistan Chaudhry Nisar Ali Khan, alimshauri Bwana Sharif kukubali uamuzi wa leo.
Mahakama imependekeza kufanyika kesi za ufisadi dhidi ya watu kadhaa akiwemo Bwana Sharif, mtoto wake wa kike Maryam na mumewe Safdar, waziri wa fedha Ishaq Dar na wengine kadhaa.
Hakuna waziri mkuu wa Pakistan aliye raia ashawai kumaliza kipindi chake cha miaka mitano.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU