Vurugu zaendelea Jerusalem

MTEULE THE BEST

Vurugu zaendelea Jerusalem

Wapalestina wawili wameuwawa katika makabiliano na jeshi la Israel hapo jana, wakati jeshi hilo lilipoizingira nyumba ya mshambuliaji baada ya vurugu zilizotokana na hatua kubwa za usalama katika eneo tete takatifu. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wake wa ndani hapo kesho likijikita katika ongezeko la vurugu baada ya Misri, Ufaransa na Sweden kutaka mkutano wa dharura wenye kujadili namna ya kufanikisha jitihada za kudhibiti vurugu za Jerusalem. Vifo hivi vya watu wawili vinatokea baada ya vitendo vya umwagikaji damu siku ya Ijumaa, ambapo kijana wa Kipalestina wa umri wa miaka 19 aliuwauwa walowezi watatu wa Kiisrael katika Ukingo wa Magharibi na Wapalestina watatu kuuliwa na jeshi la Israel. Vurugu hizo vilevile zilitokea mashariki mwa Jerusalem na katika vijiji vingine vya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi, karibu na Jerusalem

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU