MTEULE THE BEST
Wapalestina wamerudi katika eneo muhimu la kufanya ibada mjini Jerusalem kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wiki mbili baada ya Israel kuondoa vizuizi vya kiusalama.
Wanaoabudu walijaa katika eneo la jumba hilo baada ya viongozi wa Kiislamu kuondoa marufuku ya kususia ya wiki mbili kufuatia hatua hiyo ya Israel.
Mpango huo uliwekwa na Israel baada ya mauaji ya maafisa wawili wa polisi ya Israel karibu na eneo hilo.
Vizuizi vya mwisho viliondolewa siku ya Alhamisi baada ya siku kadhaa za ghasia ambapo watu saba waliuawa.
Wapalestina wamepinga kwa nguvu kuwekwa kwa vizuizi hivyo vya kiusalama ,wakidai kuwa ni jaribio la Israel kudhibiti mji huo wa zamani unaojulikana na Waislamu kama Harma al-Sharif huku Wayahudi wakiliita hekalu la mlimani.
Makundi ya raia wa Palestina walionekana wakiimba na kucheza densi katika eneo hilo kabla ya kuingia ndani kwa sala ya mchana.
Kulikuwa na ripoti za baadhi ya ghasia katika barabara nyembamba huku maafisa wa mipakani wakijaribu kudhibiti watu hao.
Vizuizi hivyo viliendelelea leo asubuhi, siku mbili baada ya mitambo ya kutambua vyuma kuondolewa.
Mzozo uliibuka baada ya polisi wawili wa Israel kuuawa karibu wiki mbili zilizopita.
Israel imesema kuwa itachukua hatua zisizokuwa na vizuizi miezi sita ijayo
Kumekuwa na makabiliano ya kila siku kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamanaji tangu mitambo ya kutambua chuma iwekwe baada ya kuuwawa kwa polisi tare 14 mwezi huu karibu na eneo hilo la Haram al-Sharif kwa waislamu na Temple Mount kwa wayahudi.
Wapalestina wanne waliuawa na raia watatu wa Israel kuuliwa kwa kuchomwa visu na Mpalesina ambaye alidai alikuwa akilipiza hatua za Israel eneo katika eneo hilo takatifu.
Maoni