MTEULE THE BEST
Zaidi ya watu 40 wameuawa wakati wa jaribio la kuwaokoa watu waliotekwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram .
Takriban watu watano wa kampuni ya kuchimba mafuta waliuawa, kwa mujibu wa chuo cha Maiduguri.
Wanajeshi pia waliuawa wakati wa uvamizi huo.
Idadi hiyo kubwa ya vifo ni pigo kwa serikali ambayo inasisitiza kuwa kundi la Boko Haram limeshindwa.
Takriban watu 20,000 wameuawa na maelfu ya wengine kutekwa tangu Boko Haram ianzishe harakati zake mwaka 2009.
Katika kisa kibaya zaidi Boko Haram waliteka wasichana 276 kutoka shule ya wasichana kaskazini mashariki mwa Nigeria ya Chibok mwaka 2014.
Tangu wakati huo wamewaachili zaidi ya wasichana 100 kubadilishana na wapiganaji.
Taarifa za kina kuhusu kile kilichotokea siku ya Jumanne hazijulikani, huku ripoti za awali kutoka kwa jeshi, zikisema kuwa watu ambao walitekwa waliokuwa ni wakifanya kazia katika chuo cha Maiduguri waliachiliwa,.
Siku ya Jumanne jeshi lilisema kuwa miili ya wanajeshi 9 na raia mmoja ilikuwa imepatikana.
Lakini sasa chuo kikuu kimesema kuwa takriban wafanyakazi watano wakiwemo wasomi wawili na dereva waliuawa wakati msafara wao uliokuwa chini ya ulinzi mkali, ulikuwa ukirejea mjini Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria
Wengine kadha hawajulikani waliko
Maoni