Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MENERA

Wanasayansi wa Uingereza wamegundua mti mrefu zaidi duniani

Chuo hicho kinasema kuwa mti huo ni mrefu zaidi ya uwanja wa kucheza soka. Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100. Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita. Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walifanya utafiti huo kwa kutumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio. Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah umepewa jina Menara ambalo linamaanisha jumba refu. Mkweaji miti kutoka eneo hilo, jami ambaye aliupima mti huo kwa kutumia kamba alisema alliogopa kuupanda mti huo ''Lakini kwa kweli picha kutoka juu ilikuwa nzuri mno. Sijui cha kusema isipokuwa tu ulikuwa uzoefu mzuri sana'', liongezea. Safari ya kuufikia mti mrefu zaidi Afrika nchini Tanzania Inadaiwa kuwa mti huo unaweza kuwa mti mrefu wenye maua duniani. Daktari Doreen B...