Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WASAFI

Mapendekezo ya sheria yatishia kazi za wasanii Uganda

Wakosoaji wa mapendekezo ya sheria mpya wanasema inalenga kuwazuwia wanamuziki kama Bobi Wine (pichani) kutoa maoni hasi juu ya maafisa Serikali ya Uganda inapendekeza sheria inayoweka masharti kwa wanamuziki wanaotoa nyimbo mpya kuziwasilisha zichunguzwe kabla ya kutolewa. Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema inalenga kuwazuwia watu kutoa maoni hasi juu ya maafisa ambao wanakerwa na umaarufu wa mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop Bobi Wine. Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36- ambaye aligeuka na kuwa mpinzani wa kisiasa , ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amepata ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana kwa kuikosoa serikali kupitia nyimbo zake. Taarifa ya mapendekezo ya sheria ya kuweka masharti kwa wanamuziki nchini Uganda imepokelewa kwa hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi wakionyesha kutokubaliana na mapendekezo hayo. Ruka ujumbe wa Twitter wa @AfricaFactsZone Africa Facts Zone@AfricaFactsZone Uganda's Government has made new outrageous and ...

Wamiliki wa WASAFI TV wajulikana, hisa za Diamond ni asilimia 45

Kituo hicho kipya cha televisheni kimezua mjadala kuhusu wamiliki wake tangu kilipoanza matangazo ya majaribio, baadhi wakisema kinamilikiwa kwa asilimia 100 na nyota huyo wa Bongo Fleva. Dar es Salaam. Ni Diamond Platnamuz au Joseph Kusaga? Ndio mjadala mkubwa uliodumu tangu mwanamuziki huyo nyota wa miondoko ya Bongo Fleva aanze kukitangaza kituo kipya cha televisheni cha Wasafi TV. Baadhi wanadai mmiliki ni Diamond na wengine wanasema Kusaga, mmoja wa manguli katika biashara ya burudani na ofisa mtendaji mkuu wa Clouds Media, wakidai anamtumia nyota huyo wa Bongo Fleva kutangaza televisheni hiyo mpya. Wakati mjadala huo ukiendelea, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA) imetoa tangazo linalodokeza majibu ya mjadala huo. Katika tangazo lake kwa umma kutaka maoni au pingamizi kuhusu maombi ya leseni ya Wasafi TV, mamlaka hiyo imewataja wamiliki watatu wa televisheni hiyo, ambayo tayari ipo hewani. TCRA imemtaja mtu anayeitwa Juhayna Zaghalulu Ajmy na ambaye ni Mtanzania, ...