Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SOMALIA

Shambulio la Kismayo: Mwandishi Hodan Nalayeh na watu kadhaa wafariki baada ya wapiganaji wa alshabab kuvamia hoteli Somalia

Kundi la wapiganaji wa al-shabab limetekeleza msururu wa mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni Takriban watu saba wameuawa katika shambulio moja la hoteli kusini mwa Somalkia ikiwemo mwandishi wa runinga mwenye uraia wa Canada na Somali Hodan Nalayeh, kulingana na ripoti. Maafisa na wale walionusurika wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga aligongesha gari lililojaa vilipuzi katika Hoteli ya Asasey katika bandari ya Kismayo kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo. Nalayeh na mumewe wameripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliouawa. Kundi la wapinganaji la al-Shabab limekiri kutekeleza shambulio hilo. Walioshuhudia wanasema kuwa walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari hilo kulipuka. Haijulikana iwapo washambuliaji hao walisalia ndani ya hoteli hiyo baada ya mlipuko huo. Afisa wa usalama Abdi Dhuhul aliambia chombo cha habatri cha AFP kwamba waziri mmoja wa utawala wa eneo hilo pamoja na wakili ni miongoni mwa waliofariki. Vyombo v...

Somalia: Mwanamume afunga ndoa na wanawake wawili wakati mmoja

Mohamed na wake zake wawili Kijana mmoja raia wa Somalia ambaye alioa wanawake wawili usiku mmoja ameambia BBC kwamba atawashawishi wanaume wengine kufanya hivyo. Bashir Mohamed anasema kuwa aliwachumbia wanawake wote kwa takriban miezi minane na kuwashawishi kufunga ndoa naye. ''Nilikuwa nikiwaleta nyumbaji wote pamoja'', aliambia BBC. ''Nilikuwa nikiwaambia wazi wote wawili kwamba nawapenda. Waliridhika'' , aliongezea. ''Umuhimu wa kuwaoa wote wawili wakati mmoja ni kwamba hawangekuwa na wivu na kwamba watajua tangu awali kwamba wamekuwa katika ndoa za uke wenza'', alisema bwana Mohammed. Alioa wanawake wawili kwa sababu alihitaji watoto wengi. ''Nitawashawishi wanaume wengi pia kufuata nyayo zangu iwapo wana uwezo'', alisema Mohamed. Ndoa za wake wengi ni halali katika utamaduni nchini Somalia lakini sio jambo la kawaida kuoa wanawake wawili wakati mmoja, kulingana na mwandishi wa BBC Mo...

Raia wa Ujerumani atekwa Somalia

Wapiganaji nchini Somalia Mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundu raia wa Ujerumani ametekwa nyara katika mji mkuu wa Somalia. Habari zinasema watu wasiofahamika waliokuwa wamebeba silaha, walimteka ndani ya eneo la ofisi hizo mjini Mogadishu na kumtoa nje kwa kutumia mlango wa nyuma, ili kuweza kuwakwepa walinzi waliokuwa katika lango kubwa la mbele. Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu amesema wana wasiwasi mkubwa na usalama wa mfanya kazi mwenzao. Amesema muuguzi huyo aliyetekwa alikuwa akifanya kazi kila siku kuokoa maisha ya baadhi ya Wasomali wenye hali mbaya