Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TCRA

Rais Magufuli apokea majina ya kuyakata mishahara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Ladislaus Matindi, ameeleza tayari ameshamkabidhi Rais Magufuli orodha ya majina ya viongozi ambao walikatisha safari zao za ndege katika shirika hilo licha ya kukatiwa tiketi za serikali. Rais Magfuli Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amedai wameshatekeleza agizo hilo la Rais Magufuli ambalo alilitoa kwenye hafla ya upokeaji wa ndege mpya ya Tanzania A220-300 aina ya Airbus. Matindi amesema “ majina ya vigogo husika tumeshayakabidhi kwa Rais, tangu tumeelekezwa tulifanyia kazi maelekezo hayo na kisha tukayakabidhi sehemu husika ,” “ Siwezi kutaja ni vigogo wa kada gani, wasiliana na Ofisi ya Rais wataweza kuwa na majina pamoja na Idara au Taasisi wanazotoka, sisi tumepeleka orodha ,” ameongeza Luhindi. Akizungumza Desemba 23, 2018 Rais Magufuli alisema “nimeambiwa pia baadhi ya tiketi huwa zinakatwa na watendaji wa serikali halafu wakati wa mwisho haw...

NDEGE YA TANZANIA AIR-BUS A220 YATUA ACCRA, KUTUA KESHO DAR ES SALAAM

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini. Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.   Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220.   “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona T...

Wema Sepetu apandishwa kizimbani

Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu leo amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili ambapo anashtakiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza video za maudhui ya ngono mitandaoni. Msanii Wema Sepetu, akiwa na mama yake mzazi Mariam Sepetu. Wema amefika mahakamani hapo majira ya saa 3 asubuhi akiongozana na mama yake mzazi, Mariam Sepetu na wakili wa msanii huyo, Reuben Simwanza, na kwenda moja kwa moja hadi kwenye ukumbi wa mahakama hiyo kusubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi yake. Shauri la kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa katika Maakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya hakimu, Maira Kasonde huku Wakili wa utetezi akiwa Ruben Simwanza na upande wa Jamhuri ukisimamiwa na Wakili Jenifer Masue, lakini imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika. Novemba 1, 2018 Wema alipandishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka l...