Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SPAIN

CORONA| EPL, LIGUE 1, BUNDESLIGA, LALIGA, UEFA, UUROPA , ITALY, N.K ZASIMAMISHWA

Coronavirus : Mechi za Ligi ya soka ya England kuahirishwa hadi tarehe 3 Aprili Mechi za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi tarehe 3 Aprili kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona. Mashindano yote Ligi ya soka ya Ulaya, mkiwemo Championi Ligi na Ligi ya Ulaya, mechi ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus. Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa. Katika Championi Ligi, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa. Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa. Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa. Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatol...

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 17.11.2019:

Gareth Bale Manchester United wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale,30, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Sun on Sunday) Paris St-Germain wanawezekana kuwa kikwazo kikubwa kwa mpango wa Manchester United wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19 mwenye thamani ya pauni milioni 120. (Sunday Express) PSG pia wanamtaka kiungo wa Liverpool Adam Lallana,31.(Sunday Mirror) Manchester United wanamtazama kwa karibu winga wa West Bromwich Albion Matheus Preira, anayecheza kwa mkopo akitokea Sporting Lisbon. (Mirror) Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho Arsenal wanajiandaa kumuwania mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uturuki, ambaye anaweza kuuzwa na Juventus kama ofa ya kuridhisha itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.(Tuttosport - in Italian) Barcelona wanajadili mkataba mpya na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32. (Mundo Deportivo - in Spanish) Mshambuli...

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 1

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 15 .07.2019: Harry Maguire, Lewis Dunk, Kieran Tierney, Leroy Sane Manchester United inalipa £80m kumsajili Harry Maguire Manchester United imeafikiana na Leicester makubaliano ya thamani ya £80m kumsajili Harry Maguire na kumfanya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia. United italipa £60m kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 26 - atakayefanyiwa ukaguzi wa kiafya leo Jumatatu - na £20m za ziada katika siku zijazo. (Sun) Leicester inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa thamani ya £45m kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (Sun) Celtic imekataa ombi la Arsenal la hivi karibuni linalokisiwa kuwa na thamani ya £25m - ili kumsajili beki wa kushoto mwenye miaka 22 Kieran Tierney. (Sky Sports) Manchester City inaamini Leroy Sane ataisusia Bayern Munich iwapo itawasilisha ombi la kumsajili winger huyo wa Ujerumani mwenye miaka 23. (Daily M...

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 11.12.2018:

Sambaza habari hii Messen Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Eden Hazard Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, tena amezungumzia kuhama kwenda Real Madrid na anasema kuwa hajui ni lini ataamua hatma yake. Lakini Mbelgiji huyo amekiri kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya huko Stamford Bridge yamekwama. (RMC Sport via Express) Mkurugenbzi wa michezo wa AC Milan Leonardo amethibitisha kuwa klabu hiyo ya Serie A imezungumza Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31. (London Evening Standard) Tottenham wamejiunga na Manchester United katika kumwinda mshambuliaji raia wa Romania Dennis Man, mchezaji huyo mwenye miaka 20 aiyechezea FCSB ambayo awali ilikuwa inajulikana kama Steaua Bucharest. (Sun) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Cesc Fabregas Spurs wanachelewa zaidi kuufungua uwanja wao mpya kutokana na ugumu wa kuandaa warsha wakati huu wa msimu wa krismasi. (Times) Meneja wa Fulham Claudio Ranieri yuko tayari kumsai...

Ronaldo amchana Messi, amtaka abadilike

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo ameibuka na kumzungumzia nyota wa Barcelona, Lionel Messi akisema angependa kumuona mchezaji huyo akicheza katika ligi kuu nchini Italia 'Serie A'. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi Cristiano Ronaldo amemhimiza mpinzani wake huyo wa muda mrefu Lionel Messi, akimtaka  "kukubali changamoto" na kumfuata nchini Italia. Alipoulizwa kama anamuhitaji Messi au la!, Ronaldo amesema, " hapana, labda yeye ndiyo ananihitaji mimi. Nimecheza Ureno, Uingereza, Hispania, Italia na kwenye timu ya taifa pia, lakini yeye bado yuko kwenye timu moja. Labda yeye kama ananihitaji mimi ". " Kwangu mimi maisha ni changamoto, ninapenda hivyo na ninapenda kuwafanya watu wangu wawe na furaha. Ningependa siku moja nayeye aje kucheza Italia kama nilivyofanya mimi, akubali changamoto, lakini kama ana furaha pale alipo ninaheshimu uamuzi wake ", ameongeza Ronaldo. Aidha Cristiano amemzungumzia Messi kama ni mchezaji mkubwa...

Luis Enrique kocha mpya wa Uhispania

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameteliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  Barcelona  Luis Enrique ametia saini mkataba  wa  miaka  miwili  kuchukua  hatamu za kuifunza  timu ya  taifa  ya  Uhispania. Anachukua  nafasi  ya  Julen lopetegui, ambaye  alifutwa  kazi katika  mkesha  wa  kuanza  kwa  fainali  za kombe  la  dunia  baada  ya  kukubali kazi katika  timu  ya  Real Madrid. Fernando Hierro alichukua  udhibiti wa  timu  hiyo  kwa  muda  kwa ajili  ya  fainali  hizo, ambapo  mabingwa  hao  wa  mwaka  2010 wa kombe  la  dunia  waliondolewa  katika  awamu  ya  mtoano na wenyeji Urusi

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.07.2018

Beki wa zamani wa Real Madrid Michel Salgado anaamini mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 24, ndiye anayelengwa na klabu hiyo msimu huu baada ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26. (Talksport) Chelsea inajaribu kuipiku Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Itali Jorginho, 26. (Manchester Evening News) City pia imembishia hodi kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, 24, huku wakiwa na wasiwasi kuhusu kumtia mkobani Jorginho. (Mirror) Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, anatarajiwa kusalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho (Bild) Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi anasema kuwa ataangazia maombi ya kumuuza kipa wa Brazil Alisson lakini kufikia sasa hakuna klabu iliowasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (FourFourTwo) Manchester United na Real Madrid wamekutana na maafisa kutoka Lazio kujadili uhamisho wa kiungo wa...