Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 15.07.2019: Harry Maguire, Lewis Dunk, Kieran Tierney, Leroy Sane
Manchester United inalipa Ā£80m kumsajili Harry Maguire
Manchester United imeafikiana na Leicester makubaliano ya thamani ya Ā£80m kumsajili Harry Maguire na kumfanya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia.
United italipa Ā£60m kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 26 - atakayefanyiwa ukaguzi wa kiafya leo Jumatatu - na Ā£20m za ziada katika siku zijazo. (Sun)
Leicester inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa thamani ya Ā£45m kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (Sun)
Celtic imekataa ombi la Arsenal la hivi karibuni linalokisiwa kuwa na thamani ya Ā£25m - ili kumsajili beki wa kushoto mwenye miaka 22 Kieran Tierney. (Sky Sports)
Manchester City inaamini Leroy Sane ataisusia Bayern Munich iwapo itawasilisha ombi la kumsajili winger huyo wa Ujerumani mwenye miaka 23. (Daily Mirror)
Tottenham na Arsenal zimejiunga na Manchester City katika kumfukuzia beki kamili wa Brazil Dani Alves mwenye umri wa miaka 36, ambaye ni ajenti huru tangu alipoondoka Paris St-Germain. (Mundo Deportivo kupitia Daily Mail)
Tottenham na Arsenal zimejiunga na Manchester City katika kumfukuzia beki kamili wa Brazil Dani Alves
Atletico Madrid haina ushahidi wa kuthibitisha tuhuma kwamba Barcelona ilikuwa na makubaliano tayari na mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, mapema mwezi Machi, kwa mujibu wa rais wa Barca Josep Maria Bartomeu. (Goal)
Mchezaji anayelengwa na Arsenal, Everton mwenye umri wa miaka 23 anayeichezea Gremio, anasema amepewa pendekezo lakini amekataa kufichua jina la klabu iliyomfuata. (Mirror)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema klabu hiyo itaendelea kuweka wazi matumaini yake kuhusu kumsajili beki wa kushoto kuichukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uskotchi Andrew Robertson, mwenye umri wa miaka 25, wakati wa dirisha la uhamisho msimu wa joto. (ESPN)
Aliyekuwa winga wa Newcastle Chris Waddle anaamini kuidhibiti Magpies itakuwa changamoto kubwa katika miaka 21 ya usimamizi wa Steve Bruce iwapo ataondoka Sheffield Jumatano kuelekea St James' Park. (Newcastle Chronicle)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Herbie Kane, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda katika klabu ya ubingwa wiki hii. Brentford, Charlton na Hull zote zinataka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20 aliyeichezea Doncaster msimu ulioipita. (Goal
Maoni