Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TANZANIA YAIKOSOA BENKI YA DUNIA

Ni kwanini Tanzania imekosoa makadirio ya benki ya dunia ya ukuaji wa uchumi wake




Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS)

Taasisi ya takwimu nchini Tanzania imesema kuwa inaweza kutathmini takwimu za ukuaji wa uchumi wake wa mwaka 2018 baada ya Benki ya dunia kutoa takwimu zilizoonyesha kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.


Waziri wa fedha wa Tanzania aliliambia bunge mwezi uliopita kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa ni 7% mwaka jana.

Benki ya dunia ambayo ilitoa hesabu zake kwa misingi ya data za taifa , matarajio ya mwaka 2019 ya ukuaji wa kiwango cha 5.4% - pia ilitoa kiwango cha chini cha ukuaji chini ya kile kilichokuwa kimekadiriwa na na serikali cha 7.1%.


Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ametetea njia zake na namna alivyofikia kiwango hicho, Reuters linaripoti.

"Tumekwenda kote nchini kukusanya data halisi , sio sawa na mtu ambaye anakaa Washington na kutengeneza sampuli za pato la ndani la nchi (GDP) kwa niaba yako,"alisema Bi Albina kulingana na Reuters

"Kwa madhumuni ya mipango ya taifa, tutaendelea kutumia data rasmi za asilimia 7.0."

Lakini maafisa nchini humo watakutana na wawakilishi wa Benki ya Dunia mwezi Agosti kuchunguza vigezo vilivyotumiwa na benki hiyo. "Kwa hiyo tunaweza kupata matokeo mengine na tathmini ya takwimu ya pato jumla la ndani la nchi -GDP ," alisema.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia uchumi wa taifa la Tanzania ulikua kwa asilimia 5.2 mwaka 2018 kulingana na benki ya dunia iliosema katika katika ripoti yake kuu mwaka huu.

Ukuaji wa mwaka uliopita uliathiriwa na kushuka kwa viwango vya uwezekazji, mauzo katika mataifa ya kigeni na ukopeshaji katika sekta ya kibinfasi, ripoti hiyo imesema.

Kulinga na Reuters, data inayohusiana na matumizi, uwekezaji na biashara inonyesha kwamba ukuaji huo ulipungua mwaka 2018.

Rais John Pombe Magufuli alianzisha mpango wa kuimarisha sekta ya viwanda baada ya kuchukua hatamu mwaka 2015, akiwekeza mabilioni ya dola katika miundo msingi, ikiwemo barabara ya reli, kufufua uchukuzi wa kitaifa wa angani pamoja na kiwanda cha umeme.


Lakini hatua ya serikali kuingilia sekta ya uchimbaji wa madini pamoja na ile ya kilimo imesababisha kupungua kwa uwekezaji katika sekta hizo katika taifa hilo linalotajwa kuwa la tatu kwa ukubwa kiuchumi Afrika mashariki, ilisema ripoti hiyo iliochapishwa na Ruters.

Kulingana na chombo hicho cha habari uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umepungua maradufu tangu 2013, huku ukuaji wa mikopo katika sekta ya kibinafsi ukipungua na kufikia chini ya silimia 4 mwaka 2018, ikiwa ni kiwango cha chini cha wastani kati ya 2013-16.

Ripoti hiyo ya benki ya dunia inajiri kufuatia ripoti ambayo haikuchapishwa ya hazina ya shirika la fedha duniani IMF mnamo mwezi Aprili ambayo pia ilihoji jinsi rais Magufuli anavyoendesha uchumi wa taifa.

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umepungua maradufu tangu 2013, huku ukuaji wa mikopo katika sekta ya kibinafsi ukipungua na kufikia chini ya silimia 4 mwaka 2018, ikiwa ni kiwango cha chini cha wastani kati ya 2013-16.

Ripoti hiyo ya benki ya dunia inajiri kufuatia ripoti ambayo haikuchapishwa ya hazina ya shirika la fedha duniani IMF mnamo mwezi Aprili ambayo pia ilihoji jinsi rais Magufuli anavyoendesha uchumi wa taifa hilo.

Katika ripoti yake, benki ya dunia WB imesema kuwa ukuaji wa kiwango cha uwekezaji ulishuka kwa sababu ya serikali kushindwa kuafikia malengo yake ya matumizi katika miradi ya maendeleo.

Ripoti hiyo inasema kwamba uchumi huo unaweza kunawiri kwa asilimia 6 kufikia 2021 iwapo kutakuwa na uimarikaji wa wa sekta ya biashara, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja mbali na uwekezaji mwengine wa kibinafsi, ilisema benki hiyo.

Viashiria vingine vya kiuchumi pia vimeonyesha kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.


Upungufu huo uliongezeka hadi asilimia 5.2 ya pato la taifa katika mwaka uliokwisha Januari 2019, kutoka asilimia 3.2 mapema mwaka mmoja uliopita.

Kwa upande mwengine , ujenzi wa reli ya kasi ya SGR na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umesaidia kuimarisha thamani ya mauzo ya kigeni yanayoingia nchini kwa asilimia 7.8%, ilisema benki ya dunia.

Benki ya Dunia imependekeza kuwa serikali inahitaji kupunguza athari za kiuchumi kupitia kuimarisha mazingira ya kibiashara na usimamizi wa fedha.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...