Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 14.07.2019: Nyemar, Odoi, Pogba, Coutinho, Maguire, Mane
Neymar alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa dau lililovunja rekodi la pauni milioni 200 mwaka 2017
Mchezaji ghali zaidi duniani wa Paris St-Germain, Neymar, amekoleza uvumi kuwa anarudi Barcelona baada ya kuachia video anayoonekana amevaa jezi ya Barca, pamoja na mistari ya biblia yenye mafumbo. (Goal.com)
Bayern Munich hawatakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji kinda wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, huku wakitarajiwa kutangaza dau la pauni milioni 45 wiki hii. (Mail)
Liverpool pia wamejiunga kwenye mbio za kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Mirror)
Barcelona ilimsajili Coutinho kutoka Liverpool kwa pauni milioni 142 Januari 2018
Kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, atakataa ofa ya kujiunga na Manchester United, akiwa na malengo ya kuelekea klabu Paris St-Germain, japo anaweza pia kukubali kurejea Liverpool.(Express)
Barcelona wamemuhakikishia wakala wa Coutinho kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo, japo anadai kuwa mteja wake anawekwa sokoni na wawakilishi walio karibu kabisa na klabu hiyo. (Sky Sports)
Manchester United hawatamuuza kiungo Mfaransa Paul Pogba kwenda Real Madrid iwapo miamba hiyo ya Uhispania watawasilisha ofa yao baada ya dirisha la usajili kufungwa kwa upande wa England, Agosti 8. (Mirror)
Beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26 - ambaye anahusishwa na uhamisho kwenda Man United kwa dau la Ā£75m - ameambia klabu yake kuwa anataka kuondoka. (Mail)
Maguire ametia nia ya kuihama Leicester kwenye dirisha hili la usajili
Maguire ameishutumu Leicester kwa kumkadiria kwa dau ghali ili asinunulike. Tayari klabu hiyo imeshazikataa ofa za pauni milioni 70 kutoka kwa United na City. (Sun)
Kiungo mchezeshaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen, 27, yawezekana akaendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya jijini London baada ya kuwa na uhaba wa klabu ambazo zimeonesha nia ya kumsajili. (Guardian)
Sadio Mane kung'oka Liverpool?
Liverpool hawajafanya mazungumzo yoyote na Real Madrid juu ya mshambuliaji raia wa Senegal Sadio Mane, 27, licha ya mkuu wa chama cha soka cha Senegal Saer Seck kudai kuwa Madrid wamepeleka ofa ya usajili. (Liverpool Echo)
Kiungo wa Everton na Senegal Idrissa Gueye, 29, amesema anafahamu juu ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho kwenda PSG lakini kwa sasa amedai malengo yake yapo AFCON. (Sport Witness)
Arsenal wapo Tayari kuminyana na Tottenham na Juventus katika mbi za kumsajili kiungo waklabu ya Roma ya Italia Nicolo Zaniolo, 20. (Calciomercato)
Liverpool pia wamejiunga kwenye mbio za kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Mirror)
Maoni