Ruka hadi kwenye maudhui makuu

URUSI: KUCHUNGUZA ANGA ZA JUU



Urusi yazindua darubini ya kudhibiti joto la anga



Chombo cha Spektr-RG kimetengenezwa kwa muundo wa darubini mbili ndani ya chombo kimoja

Moja ya safari muhimu zaidi za kisayansi nchini Urusi kuwahi kushuhudiwa katika baada ya utawala wa utawala wa Kisovieti imezinduliwa kutoka eneo la Baikonur.

Spektr-RG telescope chenye darubini ya anga za mbali -ni uvumbuzi uliokamilika kwa ushirikiano na Ujerumani ambayo inatarajia kupima nishati ya joto kote angani na kutoa taarifa.


Watafiti wanasema taarifa hii itasaidia kupata muundo wa dunia kwa upana zaidi.

Matumaini ni kwamba Spektr-RG kitaweza kutoa mtizamo mpya juu ya upana wa anga.


Utengenezaji wa chombo hiki ni safari ya miongo kadhaa kwa wanasayansi wa urusi

Kinatarajiwa pia kutambua idadi ya mpya ya vyanzo vya nishati , kama vile mashimo makubwa meusi yaliyopo katikati mwa nyota nyingi.

Wakati gesi inapoanguka katika mashimo hayo , huwa na joto kali na kumeguka na kugeuka kuwa joto kali.


Mionzi yake hatimae husababisha hali mbaya ya joto kwa dunia.

Darubini ya Spektr-RG inatarajiwa kugundua labda mashimo milioni tatu makubwa sana meusi angani wakati wa itakapokuwa angani hadi mwisho wa maisha yake.


Kuanzishwa kwa safari hii kumecheleweshwa katika wiki za hivi karibuni kutokana na masuala ya kiufundi yanayohusiana na roketi za safari za anga

Darubini hiyo inazunguka juu ya uzio (orbit) uliopo kwenye roketi ya Proton ambayo iliondoka Baikonur Cosmodrome eneo la Kazakhstan saa sita na dakika 31 kwa saa za Kazakhstan.

Itachukua hata hivyo wiki nyingi kabla ya darubini hiyo kuanza kazi yake.

Chombo hicho cha anga za mbali kitatakiwa kusafiri katika eneo linalochunguzwa zaidi yapata kilomita milioni 1.5 kutoka duniani linalofahamika kama -Lagrange Point 2.

Ni hapa ambapo chombo cha Spektr-RG kinaweza kupata mazingira thabiti bila kuwa nakivuli na kuyumbishwa na joto ambalo vinginevyo lingekipata kama kingekuwa karibu na sayari yetu dunia.

Spektr-RG kimetengenezwa kwa muundo wa darubini mbili kwa pamoja.


Chumba kinachochukua nafasi kubwa katika chombo hiki cha darubini ya anga za mbali, ukipenda spacebus au chassis, ni mfumo uliotengenezwa Ujerumani wa eRosita na karibu yake umefungwa na kifaa cha kisayansi kilichotengenezwa na Urusi kinachofahamika kama ART-XC.

Vifaa vyote hutumia kundi la muduli za kioo kudhibiti nguvu za mwangaza kwenye kamera za ung'amuzi.


Kikundi cha vioo saba huielekeza mtango wa kupima joto kwenye kamera ya ug'amuzi wa taarifa

eRosita na ART-XC zitachukua ramani ya miale kadri inavyosambaa angani katika ukubwa wa nguvu za kati ya 0.2 hadi 30 katika kipimo cha nguvu za kasi ya nishati ya anga- kiloelectron volts (keV).

Katika kipindi cha miezi sita, watatakiwa kuwa waChombo cha anga cha China huenda kikadondoka ''karibuni'' mekamlishia uchunguzi wa anga yote, ambao utarudiwa tena na tena kupata usahihi wa taarifa.

Wanasayansi wanatarajia taarifa/data zitafichuliwa.


Vipimo vitakapokamilika, uchunguzi unaweza kuendela kwa kuchukua nakili za picha ya anga.

Lengo kuu la chombo cha Spektr-RG litakuwa ni kuchunguza sehemu za anga zinazotambuka kama ''kitu cheusi'' au "nishati nyeusi".

Sehemu hii ya anga inachukua hadi 96% ya shemu ya uwiano wa duniani.

Ufahamu wa Spektr-RG utatokana na picha ya ramani ya mgawanyo wa joto kali la inayochoma linalotolewa angani

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.