Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 16.07.2019:Maguire, Neymar, Bruce, Fernandes, Alderweireld, Coutinho
Leicester imemwambia mlinzi wake wa kati Harry Maguire, 26, kuwa anaweza kuondoka (Telegraph)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, amerejelea kauli yake uhusu nia yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo kwenye mkutano wake na mkurugenzi wa ufundi Leonardo . (ESPN)
Newcastle watalipa pauni milioni 4 kama fidia kwa timu ya Sheffield Wednesday kwa ajili ya kocha wao wa zamani Steve Bruce.(Sun)
Wasaidizi wa Bruce Steve Agnew na Stephen Clemence pia wameondoka Sheffield Wednesday na watajiunga naye St James'Park .(Newcastle Chronicle)
Manchester United watapeleka rasmi ofa ya kumnasa kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, katika kipindi cha majuma matatu yajayo.
Mkurugenzi wa Roma Gianluca Petrachi amethibitisha kuwa klabu yake ina mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Tottenham Toby Alderweireld, 30. (Football Italia)
Alderweireld na mchezaji mwenzake Christian Eriksen, 27, wanajiandaa kusafiri kwenda Singapore na klabu siku ya Jumatano, ingawa kumekuwa na maswali kuhusu mustakabali wao.(London Evening Standard)
Kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, huenda akarejea Liverpool kwa mkataba wa miaka miwili kwa mkopo, huku timu hiyo yenyewe ikiwa na mipango ya kumnunua kwa pauni milioni 88.(Calciomercato, via Sport Bible)
Bayern Munich imekata matumaini ya kumalizia dili la pauni milioni mmoja kumnasa winga wa Manchhester City Leroy Sane, 23.(Sky Germany, via Mail)
Arsenal imeendelea kuwa na mazungumzo na Celtic kuhusu dili la kumpata beki wa kushoto Kieran Tierney .(London Evening Standard)
Inter Milan wana shaka kuhusu kitita cha pauni milioni 75 Manchester United inakihitaji kwa ajili ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku.Inter imetoa ombo la mkopo wa miaka miwili, ambapo wataweza kulipa kwa awamu za Pauni milioni 9, pauni milioni 27 na pauni milioni 27, lakini United wanataka fedha zote kwa mkupuo. (Star)
West Ham wako kwenye mazungumzo wakitaka saini ya mshambuliaji Sebastien Haller, 25. (London Evening Standard)
Wolves wako na mipango ya kumsajili Wallace, 24,mlinzi wa Lazio (Birmingham Mail)
Gatasaray wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa magwiji wa ligi ya Serie A, AC Milan ili kumpata kiungo wa Fulham Jean Mchael Seri, 27 . (Fanatik, via Sport Witness)
Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anatazama uwezekano wa kuhamia Bundesliga. (Independent)
Maoni