Donald Trump ashutumiwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya wabunge wa Democratic
Rashida Tlaib (kati), akiwa na Alexandria Ocasio-Cortez (kushoto) na Ayanna Pressley (kulia)
Rais wa Marekani Donald Trump ameshutumiwa kwa ubaguzi wa rangu baada ya kundika ujumbe kwenye twitter akiwashambulia wabunge wanawake wa chama cha Democratic.
Amedai kuwa wanawake hao "wamewasili kutoka mataifa ambayo serikali zake ni majanga matupu", kabla ya kupendekeza "warudi walikotoka".
Baada ya hapo alisema kuwa spika Nancy Pelosi "atafurahi sana kuwashughulikia kwa haraka mipango ya safari ya bure".
Haya ni wiki moja baada ya Bi Pelosi kukabiliana kwa maneno na "kundi hilo", la wabunge wasio watu weupe wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democratic.
Kati ya wabunge hao wanne, watatu - Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib na Ayanna Pressley - walizaliwa na kulelewa Marekani, huku wanne, Ilhan Omar, alihamia Marekani alipokuwa mtoto.
Bi Ocasio-Cortez alizaliwa mjini Bronx - New York, kiasi cha maili 12 kutoka hospitali ya Queens alikozaliwa Trump mwenyewe.
Rais Trump amesema nini?
Katika msururu wa ujumbe kwenye twitter, Trump amewashutumu wabunge hao kwa kumshutumu yeye na Marekani kwa "ukali".
Aliandika: "Inavutia kuona wabunge wa Democratic 'wanaotaka maendeleo' ambao waliwasili kutoka nchi ambazo serikali zake ni majanga matupu, zilizo mbaya zaidi, zilizo na kiwango kikubwa cha rushwa, na zisizojiweza kokote duniani (iwapo ni serikali zilizokuwa zinafanya kazi) sasa wakizungumza kwa ukali wakiwaambia watu wa Marekani, taifa kubwa na lenye nguvu duniani, namna tunavyostahili kuiendesha serikali yetu.
"Kwanini wasirudi kusaidia kuyarekebisha mataifa yaliosambaratika na yaliogubikwa kwa uhalifu wanakotoka. Alafu warudi watuonyeshe namna inavyostahili kushughulikiwa.
"Maeneo hayo yanhitaji usaidizi wenu sana, mungeondoka haraka sana. Nina hakika Nancy Pelosi atafurahi sana kuwashughulikia mipango ya safari ya bure!"
Hakuwataja moja kwa moja wabunge wanawake waliokuwa akiwazungumza.
Hatahivyo, kutokana na kumtaja Bi Pelosi imedhaniwa pakubwa kwamba anamaanisha Bi Ocasio-Cortez, Bi Tlaib, Ms Pressley na Bi Ms Omar.
Katika wiki iliyopita, Pelosi amekabiliana kwa maneno na Bi Ocasio-Cortez, aliyemshutumu kwa kuwashutumu wanawake wa rangi kufuatia tofauti kati ya Democrat kuhus mswada wa usalama wa mpakani.
Kauli hiyo imepokewaje?
Bi Pelosi, spika wa bunge, amenukuu ujumbe wa Trump na kutaja maneno yake ya "kibaguzi".
"Wakati @realDonaldTrump anawaambia wabunge wanne wa Marekani warudi nchini mwao, anthibitisha mpango wake wa 'Make America Great Again' unahushu kuifanya Marekani liwe taifa ka watu weupekwa mara nyingine," alisema.
"Utofauti wetu ndio nguvu yetu na umoja wetu ndio nguvu zetu," amesema.
Bi Tlaib, mbunge wa Michigan 13th district, alituma ujumbe akitaka kura ya kutokuwana imani na Trump iidhinishwe.
"Unataka jibu kwautovu wa sheria na kushindwa kwa rais ? Yeye ndiye janga. Mitazamo yake ndiyo janga, anahitaji kura ya kutokuwana imani naye" aliandika.
Bi Ocasio-Cortez alimtumia Trump ujumbe: "zaidi ya kutokubali kuwa Marekani imetuchagua, huwezi kukubali kwamba hatukuogopi."
Bi Omar alimwambia rais kwamba "anapalilia utaifa wa watu weupe kwasbaabu una hasira kuwa watu kama sisi wanalitumikia bunge na kupambana dhidi ya ajenda yako ya chuki".
Kadhalika alimuita "kiongozi mbaya, mfisadi mkubwa na kiongozi asiyeweza kuwajibika tuliyewahi kumuona".
Na Bi Pressley alituma picha aliyonasa ya ujumbe wa Trump akiongeza: "HIVI ndivyo ubaguzi wa rangi ulivyo Sisi ni demokrasia ilivyo."
Wanachama wa Democratic wanaowania uteuzi wa urais pia walimshutumu Trump. Seneta Elizabeth Warren alisema "kauli chafu" ni "shambulio la kibaguzi".
Bernie Sanders pia alimshutumu Trump kwa ubaguzi
Wabunge wachache wa Republican walituma ujumbe moja kwa moja ila binti yake John McCain anayekiunga chama hicho mkono Meghan McCain -alisema: "Huu ni ubaguzi wa rangi."
Wachambuzi wengine pia walishutumu katika mitandao ya kijamii.
Maoni