Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya JPM

Sababu za Rais Magufuli kusitisha sherehe ya Uhuru

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9, 2018 na kuagiza kuwa fedha zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya kufanikisha shamrashamra hizo ameelekeza zitumike kujenga hospitali mkoani Dodoma ambayo itaitwa Uhuru Hospitali. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumanne, Novemba 20, 2018 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Dkt. Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mkoani Dodoma. Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Lindi pamoja na Wilaya zake katika kikao cha maandalizi ya shughuli za kuzima Mwenge kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Amesema hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo na Chamwino  kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam itakuwa inawahudumia wakazi w...

BREAKING: Rais Magufuli Kaagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, OCD, Mkuu wa Upelelezi, Mkuu wa Kituo Kyerwa Wasimamishwe Kazi

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kyerwa Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa Robert Marwa.  Viongozi hao wa Polisi wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika Wilaya ya Kyerwa pamoja na tuhuma nyingine.  Aidha,Rais Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mej. Jen Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa endapo watabainika kuhusika katika magendo ya kahawa na makosa mengine kwa mujibu wa sheria.  Tuhuma dhidi ya viongozi wa polisi katika Wilaya ya Kyerwa zimebainika  wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Maja...