Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU AZURU CHUO KIKUU CHA KILIMO BELARUS

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Belarus (Belarusian State Agrarian Technical University - BSATU) na kufanya mazungumzo na viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Bw. Romaniuk Nikolai.   Mazungumzo hayo yamefanyika leo (Jumatano, Julai 23, 2025) kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho jijini Minsk ambapo masuala ya ushirikiano baina ya vyuo vikuu vya Tanzania vikiwemo vya Sokoine na DIT yalijadiliwa.   Waziri Mkuu aliwaeleza viongozi wa chuo kikuu hicho jinsi Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyoboresha sera ya elimu ambayo inataka elimu ya amali na stadi za ufundi ziwe sehemu muhimu katika mitaala ya mafunzo yanayotolewa nchini kote.    Aliwaeleza viongozi hao juu ya hati ya makubaliano kwenye sekta ya elimu iliyosainiwa jana mbele ya Waziri Mkuu wa Belarus na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuangalia namna ya kuandaa ziara za mafunzo, kubadilishana wanafunzi na wahadh...