Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KENYA

BONIFACE MWANGI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO 21

Picha
Mwanaharakati mashuhuri anayetetea haki za binaadamu nchini Kenya, Boniface Mwangi atafikishwa Mahakamani kesho Jumatatu Julai 21 kwa madai ya kuchochea vitendo vya Kigaidi. Idara ya Polisi nchini Kenya imethibitisha kumkamata Boniface kwa madai ya kuitisha maandamano yaliyokuwa na vurugu ya kupinga Serikali ya Rais Ruto. Idara ya upelelezi nchini Kenya, DCI imesema katika mtandao wake wa X kwamba maafisa wake wamemkamata Mwangi nyumbani kwake katika kaunti ya Machakos na kupata Mabomu mawili ya kutoa machozi, Mkanda wa risasi, simu mbili za mkononi, Kompyuta na vijitabu kadhaa vya kutunza kumbukumbu. Boniface Mwangi pia anapaswa kusimamishwa kizimbani kujibu makosa ya kumiliki Silaha kinyume cha sheria. Taarifa za kukamatwa kwake tayari zimezua hasira miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakitaka mwanaharakati huyo kuachiwa huru bila masharti.

Polisi wa Kenya Wapiga Marufuku maandamano ya Upinzani

Picha
Polisi nchini Kenya wamepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatatu jijini Nairobi.  Maandamano yaliyopendekezwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ni kinyume cha sheria, kulingana na Inspekta Mkuu wa Polisi Japhet Koome.  Kile ambacho serikali iliita maandamano yasiyoidhinishwa katika miji kadhaa ya Kenya Jumatatu iliyopita yaligeuka kuwa ghasia, na kuua mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na kujeruhi wengine kadhaa.  Waandamanaji waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia nje ya ofisi za serikali katika mji mkuu na kuchoma matairi barabarani.  Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na kuwakamata viongozi watatu wa upinzani na zaidi ya waandamanaji 200.

RAIS WA TANZANIA ATOA TAHADHARI KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORANA

Picha
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani. Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana ya jeshi hii leo jijini Dar Es Salaam. Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo. ''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.'' ''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua na hatua zimeanza kuchukuliwa waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''. ''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga...

MTANZANIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MAISHA KENYA

: Mahakama jijini Nairobi imewahukumu washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio la mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa. Miongoni mwa waliohukumiwa ni Rashid Charles Mbeserero anayetuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, wengine waliohukumiwa na Mtanzania huyo ni  Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar ambao wao wamehukumiwa kwenda jela miaka 41 kila mmoja. Wote walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa Kundi la Al-Shabab.Takriban wanafunzi 148 walifariki dunia katika shambulio hilo. Hukumu hiyo imepitishwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa watatu hao ni wanachama wa Kundi la Al-shabab kutoka Somalia

Waabiri ndege kisiri 'stowaway' huponea?

Picha
Mshukiwa aliyeabiri ndege kisiri inaaminika ameanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways  kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, na kuanguka katika bustani moja huko kusini mwa London Lakini ni mara ngapi visa kama hivyo huhuhudiwa na hali huwa vipi wakati wa safari za aina hiyo? Ni mara ngapi visa hivi hutokea? Licha ya kwamba sio jambo la kawaida, hii sio mara ya kwanza kwa mtu kuingia katika sehemu za ndege wakati ndege hiyo ikisafiri na kujificha wakati wa safari ya kuelekea Uingereza. mwili ulipatikana katika bustani ilioko Offerton Road huko Clapham Kati ya Januari 2004 na Machi 2015, watu sita walioingia kwa siri katika ndegekatika uwanja wa ndege Uingereza walipatikana kwa mujibu wa  takwimu za hivi karibuni za shirika la viwanja vya ndege (CAA ). Mwingine mmoja alipatikana katika ndnai ya ndege ya Uingereza katika uwanja wa ndege ng'ambo. Takwimu kutoka shirika la viwanja vya ndege Marekani zimeashiria kuwa watu 96 wamewahi kujificha katika sehemu za ndege ...