BONIFACE MWANGI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO 21


Mwanaharakati mashuhuri anayetetea haki za binaadamu nchini Kenya, Boniface Mwangi atafikishwa Mahakamani kesho Jumatatu Julai 21 kwa madai ya kuchochea vitendo vya Kigaidi.


Idara ya Polisi nchini Kenya imethibitisha kumkamata Boniface kwa madai ya kuitisha maandamano yaliyokuwa na vurugu ya kupinga Serikali ya Rais Ruto.


Idara ya upelelezi nchini Kenya, DCI imesema katika mtandao wake wa X kwamba maafisa wake wamemkamata Mwangi nyumbani kwake katika kaunti ya Machakos na kupata Mabomu mawili ya kutoa machozi, Mkanda wa risasi, simu mbili za mkononi, Kompyuta na vijitabu kadhaa vya kutunza kumbukumbu.


Boniface Mwangi pia anapaswa kusimamishwa kizimbani kujibu makosa ya kumiliki Silaha kinyume cha sheria.


Taarifa za kukamatwa kwake tayari zimezua hasira miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakitaka mwanaharakati huyo kuachiwa huru bila masharti.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU