FAHAMU KWANINI MWANAUME HUMWAGA SHAHAWA USIKU AKIWA AMELALA/USINGIZINI.
Mwanaume kumwaga mbegu akiwa usingizini huitwa ndoto nyevu (nocturnal emission) au kwa lugha ya kawaida kumwaga bila kukusudia usiku.
Hili ni jambo la kawaida, hasa kwa wanaume vijana na hata watu wazima. Sababu kuu huwa ni za Kisaikolojia, Maumbile na hata Mihemko ya mwili.
Nimekuwa naletewa kesi hii na Wanaume wakijua labda ni Matatizo yao ya Ki-Afya au laa Wanavamiwa na Majini mahaba.
Ni kweli kuna nafasi ya kuvamiwa na Pepo wa ngono hao jini mahaba lakini pia kuna pepo wa Kingono wajulikanao kama Sexual Transmitted Demons huwavamia Wanaume kwa wanawake pia lakini njia hii huwa ni tofauti na kuota ndoto nyevu.
Zifuatazo ni Sababu za kwanini Mwanaume Humwaga Mbegu za Kiume akiwa Usingizini ama laa akiwa amelala hata inapokuwa Mchana.
1. Kwanza ni matokeo ya Mwili Kujisafisha.
Mwili wa Mwanaume hutengeneza mbegu (manii) kila siku, Kama hajafanya tendo la ndoa wala kufanya punyeto yaani kujichua kwa muda mrefu mwili hujitoa presha kwa njia ya kumwaga mbegu akiwa usingizini.
2. Pili huwa ni Ndoto za Kihisia (Erotic Dreams) Nyege.
Wakati mwingine Mwanaume anaota ndoto za kimapenzi, ambazo husisimua mwili wake hata bila kuguswa, Mwili unavyojisikia kuwa na hamu, unaweza kusababisha mshindo (orgasm) akiwa usingizini.
3. Tatu huwa ni Mabadiliko ya Homoni.
Kwa vijana waliobalehe na wanaume walio katika umri wa nguvu za kiume yaani wamepevuka, viwango vya homoni ya testosterone huwa juu.
Na hali hii huongeza uzalishaji wa shahawa na msisimko wa mara kwa mara hata bila sababu ya moja kwa moja kwa Mwanaume.
4. Inne huwa ni kulikosa Tendo la Ndoa kwa Muda Mrefu.
Mwanaume anapokosa kushiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu, mwili huchukua hatua ya "kuji-relax" kwa kutoa mbegu kupitia ndoto nyevu kama njia ya kupunguza mkusanyiko wa shahawa.
5. Tano huwa ni Msongo wa Mawazo au Mihemko ya Kihisia.
Wakati mwingine msongo wa mawazo au kufikiria sana mambo ya kimapenzi kunaweza kuathiri ndoto na hatimaye kusababisha kumwaga mbegu akiwa usingizini.
Pengine unajiuliza Je ni Tatizo?.
Hapana Ndoto nyevu si tatizo Ki-Afya huwa ni jambo la kawaida kwa Wanaume wengi, hasa waliobalehe na hata kwa watu wazima hutokea.
Kama haitokei mara kwa mara kiasi cha kusababisha uchovu au maumivu, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi unachopaswa ni kutulia tu bila wasiwasi.
Maoni