Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel atakuwa mwenyeji wa waziri mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglo kwa mazungumzo wakati nchi hizo mbili zikijaribu kumaliza mzozo wa tofauti zao. Mahusiano kati ya washirika hao wa jumuiya ya kujihami ya NATO yamevurugika kwa kiasi kikubwa , hususan tangu pale lilipofanyika jaribio lililoshindwa la mapinduzi nchini Uturuki mwaka 2016 na kuanza ukandamizaji ambao ulishuhudia mamia kwa maelfu ya watu wakikamatwa, ikiwa ni pamoja na Wajerumani kadhaa ama wale wenye uraia pacha. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel Ujerumani ambayo ina wakaazi milioni tatu wenye asili ya Uturuki , mwaka jana iliwashauri...