MTEULE THE BEST
Watu duniani waukaribisha mwaka 2018 kwa Sherehe
Watu kote duniani wameukaribisha mwaka mpya wa 2018 kwa sherehe mbali mbali zikiwemo kufyatua fataki na kushiriki ibada maalum. Miongoni mwa nchi zilizoukaribisha kwanza mwaka huu mpya ni Australia ambako fataki ziliwashwa katika jengo maarufu la Sydney Opera.Hapa Ujerumani sherehe za kuukaribisha mwaka mpya zilifanyika chini ya usalama mkali kuepusha matukio ya uvunjaji sheria kama ilivyoshudiwa miaka miwili iliyopita ambapo wanawake walinyanyaswa kingono katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Cologne. Polisi mjini Berlin iliongeza askari 1,600 wa kushika doria.Hii leo Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ataendesha misa katika ukumbi wa Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican ambako atahimiza kuwepo amani duniani na kuhimiza ujumbe wa kuwajali wasiobahatika katika jamii hasa wahamiaji na wakimbizi.
Ulimwengu unapoendelea kusherehekea kufika kwa mwaka mpya wa 2018, sherehe za aina yake zimekuwa zikifanyika miji mbalimbali mashariki hadi magharibi.
Picha hizi ni za jinsi hali ilivyokuwa miji mbalimbali.
Maoni