Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel atakuwa mwenyeji wa waziri mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglo kwa mazungumzo wakati nchi hizo mbili zikijaribu kumaliza mzozo wa tofauti zao.
Mahusiano kati ya washirika hao wa jumuiya ya kujihami ya NATO yamevurugika kwa kiasi kikubwa , hususan tangu pale lilipofanyika jaribio lililoshindwa la mapinduzi nchini Uturuki mwaka 2016 na kuanza ukandamizaji ambao ulishuhudia mamia kwa maelfu ya watu wakikamatwa, ikiwa ni pamoja na Wajerumani kadhaa ama wale wenye uraia pacha.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel
Ujerumani ambayo ina wakaazi milioni tatu wenye asili ya Uturuki , mwaka jana iliwashauri wawekezaji wake pamoja na Wajerumani wanaokwenda Uturuki kwa ajili ya mapumziko ya likizo kuepuka kwenda nchini humo na kutaka kupunguzwa kwa fedha zinazotolewa kwa Uturuki kutoka katika Umoja wa Ulaya zinazohusishwa na mazungumzo yaliyokwama ya uanachama.
Hata hivyo , Uturuki katika wiki za hivi karibuni imetuma ishara kadhaa kwamba inataka kurejea katika mahusiano bora na Umoja wa Ulaya na Ujerumani, katika wakati ikiwa katika uhusiano tete na Marekani, Israel na baadhi ya mataifa ya ghuba.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan , kwa kutangaza mwezi uliopita kwamba Uturuki "inalazimika kupunguza idadi ya maadui zake na kuongeza idadi ya marafiki", alikutana na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa mjini Paris Ijumaa(05.01.2018).
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na rais wa Uturuki Tayyip Erdogan
Akiongeza uhusiano wa binafsi katika mazungumzo ya Jumamosi, Gabriel amemwalika waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki katika mji anakotoka wa Goslar, baada ya viongozi hao wawili kukutana mwezi Novemba katika mji anakotoka Cavusoglo katika jimbo la kusini la Antalya.
Matembezi ya pamoja
Kufuatia taarifa za vyombo vya habari jana, Gabriel atamchukua mgeni wake kwa matembezi katika mji wa kale ambao umeorodheshwa kuwa ni turathi wa Goslar , ulioko karibu na brunswick katika milima ya Harz.
Casovuglo katika uhariri wa gazeti jana Ijumaa ametaka kumalizika kwa kile alichokiita "diplomasia ya kupigizana kelele" baina ya Uturuki na Ujerumani na kuanza "mwanzo mpya" ulio katika msingi wa urafiki na ushirikiano kati ya "washirika sawa".
Ujerumani pia ilitaka ukaribiano wa "hatua kwa hatua" na kusema mazungumzo ya Jumamosi yataangalia masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na "matatizo", msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni amesema.
Mwandishi habari Deniz YĆ¼cel ambaye yuko kizuwizini nchini Uturuki
Kikwazo kikubwa hivi sasa ni kuwekwa kizuwizini kwa mwandishi wa gazeti la Die Welt mwenye uraia wa Uturuki na Ujerumani Deniz Yecel kwa madai ya ugaidi tangu Februari mwaka jana, na Wajerumani wengine sita ambao serikali inasema wamefungwa kwa "sababu za kisiasa".
Uturuki katika wiki za hivi karibuni imewaachia huru Wajerumani kadhaa ambao Gabriel amewaeleza kuwa ni "mateka", miongoni mwao ni mwandishi habari Mesale Tolu.
Matumaini yaongezeka kwa watu walioko kizuwizini
Matumaini yameongezeka kwamba kesi ya Yucel pia inaweza kutatuliwa baada ya serikali ya Uturuki wiki hii kuishughulikia kwa mara ya kwanza katika miezi 10 kwa kuipeleka katika mahakama ya katiba, ambayo hivi karibu itaamua iwapo kumwachia kutoka katika kizuwizi cha kabla ya kuanza kwa kesi.
Casovuglo amesisitiza uhuru wa mahakama za Uturuki lakini ameahidi kwamba "tunafanya kila liwezekanalo katika madaraka yetu ya kisiasa kuharakisha mahakama kuchukua hatua".
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu
Mzozo kati ya nchi hizo mbili katika miaka ya hivi karibuni umechochewa na mizozo mingine, kuhusiana na mchekeshaji wa televisheni ya Ujerumani alipomkashifu Erdogan, azimio la bunge la Ujerumani mwaka 2016 kuhusiana na mauaji ya kimbari ya Warmenia, na Uturuki kukataa ziara zilizokuwa zifanywe na wabunge wa Ujerumani katika vituo vya kijeshi nchini Uturuki.
Uturuki imeishutumu Ujerumani kwa kushindwa kuwakamata wafuasi imamu anayeishi Marekani Fethullah Gulen , ambayo nchi hiyo inamshutumu kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi la mwaka 2016, na kushindwa kuwazuwia wanamgambo wa Kikurdi.
Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi. Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria. Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao. Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...
Maoni