Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 4, 2018

Makala: Achana na Wasafi Festival; Diamond, Alikiba hadi Studio

Huwenda nyakati zikawalazimu Diamond Platnumz na Alikiba kuwa kitu kimoja kwenye muziki kwa sasa. Ni kipindi kirefu wameripotiwa kutoelewa ingawa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hilo.  Kwa sasa Diamond yupo katika pilika pilika za kuhakikisha tamasha lake la Wasafi Festival linafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wakati akieleza kuhusu ujio wa Wasafi Festival alieleza kuwa angetamani na Alikiba angekuwepo kitu ambacho kiliibua mjadala mpana zaidi.  Alikiba tayari amekubaliwa kuwa sehemu ya udhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Wengi wamesema huu ni mwanzo nzuri kwa wasanii hawa kurudisha ushirikiano wao na kufanya vitu vikubwa zaidi.  Kwanini Studio    Hapo jana Diamond Platnumz akiwahojiwa na kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya alisema si Alikiba kushiriki Wasafi Festival tu bali hata kufanya wimbo pamoja yupo tayari.  "sio tu Alikiba mtu yeyote ambaye anahisi kuna sehemu nikimuweka Diamond itanisaidia katika k...

Rais Magufuli kutuma barua kwa Waziri Mkuu wa Israel

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameandika barua ambayo itapelekwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Israel Benjamin Netanyahu kwaajili ya shukrani kwa kutambua mchango wa taifa hilo kwa Tanzania.   Rais Magufuli amesema hayo leo Novemba 8, alipokutana na timu ya wataalamu wa matibabu ya moyo kutoka nchini Israel na Marekani, Ikulu Jijini Dar es salaam, wataalam hao wanashirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.  "Nimeandika barua ambayo nitakukabidhi Balozi, umpelekee Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu inayoeleza namna ninavyokubali utendaji kazi wake, najua hii barua itamfikia ili kuonesha kazi nzuri mliofanya," amesema Rais Magufuli.  "Niwaombe Madaktari na Wataalamu kutoka Israel mkija msije tu kwa masuala  ya Udaktari siku nyingine mnaweza mkaja kwa masuala ya kufurahi,  mnaenda Serengeti National Park, Ngorongoro na maeneo mengine ambayo ni  ya kuvutia".  Madaktari hao zaidi ya thelathini wamekuja nc...

Mambo 10 usiyofahamu kuhusu Hamisa Mobetto

Mrembo Hamisa Mobetto amejizolea umaarufu mkubwa kwenye kazi yake ya mitindo na urembo, hadi sasa kwenye muziki wa Bongo Fleva. Haya ni mambo 10 ya kawaida ambao huyafahamu kuhusu mrembo huyo.  1. Sauti ya Hamisa Mobetto ndio inasikaka kwenye wimbo wa Diamond Platnumz, Lava Lava na Mbosso uitwao Jibebe.  Sauti ya mwanamke inayosikika 'I like ndio ya Hamisa.  2. Kwa miaka miwili mfululizo Hamisa Mobetto ameshinda tuzo ya  Starqt Awards ambazo hutolewa nchini Afrika Kusini.Mwaka 2017 alishinda kupitia kipengele  cha People Choice Awards, pia aliwania kwenye kipengele cha Super Mum. Starqt Awards ni tuzo zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine.  3.Tangu akiwa mdogo Hamisa anakiri kuwa alipenda sana muziki na alitamani kuwa mwanamuziki. Kutokana na mahaba yake kwenye fedha akajikuta ameingia kwenye movie na mitindo.  4. Mashabiki wengi wanajua kuwa wimbo wa kwanza Hamisa Mobetto kurekodi ni Madam Hero kutokana ndio wa kwanza kutoka...

Rais Donald Trump kukutana na Rais Putin katika mkutano wa G-20

Rais wa Marekani Donald Trump afahamisha kuwa atakutana na rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa G-20, mkutano ambao unatarajiwa kufanyika nchini Argentina.  Mkutano wa G-20 utafanyika mwishoni mwa Novemba.  Rais Trump ametoa taarifa hiyo katika mahojiano aliofanya na waandishi wa habari mjiniikulu mjini Washington.  Trump atashiriki pia katika hafla ya maadhimisho ya kusitishwa vita  ya mwaka 1918 mjini Paris nchini Ufaransa Novemba 10 n a 11

Mtoto wa siku mbili atupwa kandokando ya ziwa Victoria

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kumuokota mtoto mmoja wa kike akiwa hai anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 2 hadi 3 baada ya kutupwa kichakani kandokando mwa ziwa Victoria na mtu asiyefahamika maeneo ya Bwiru ziwani Wilayani Ilemela.  Tukio hilo limetokea Novemba 1, 2018  hii ni baada ya watu waliokua wakipita njiani kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani ndipo walifuatilia na walipoona ni mtoto walitoa taatifa Polisi.  Polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta mtoto wa kike akiwa ametupwa kichakani hapo akiwa hai huku mwili wake ukiwa umeviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.  Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Mtoto huyo amepata matibabu na hali yake inaendelea vizuri amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru Wilayani  Ilemela kwa ajili ya hifadhi.  Hata hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mama wa mtoto huyo

Ijue Siri Ya Kuondokana Na Ukata

Siku ya leo katika pekua pekua zangu za kuongeza chakula cha ubongo nilikutana na kauli ambayo kiukweli ilifanya mishipa yangu ya ardenalini kuweza kushtuka kwa kasi kama vile nimeona kitu cha hatari sana.  Kauli hiyo ilikuwa na maneno mawili yenye kubeba ujumbe mzito ambao sina uhakika kama, ujumbe huo upo mzani ambao ataweza kupima kilo zake, hii ni  kutokana na uzito uliopo katika ulipo katika ujumbe huo,  labda ujumbe huo upimwe na kichwa cha mwanadamu mwenye mtazamo chanya ndio anaweza kuuelewa.  Ujumbe huo unasema “unachokiogopa ndicho kitakachokua” narudia kusema tena unachokiogopa ndicho kitakachokua. Kwa haraka haraka unaweza usielewe maana ya msemo huo ila pindi utulizapo fikra ya ujazo wa akili unaweza kuelewa.  Binafsi nilichokielewa katika kauli hii ni kwamba, moja kati changamoto kubwa ambayo huwazuia watu wake kutoweza kutimiza makusudio yao hapa dunia ni kitu ambacho tunachokiita ni woga.  Woga ndio ambao umekua tatizo...