Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya VITA BARIDI

Umoja wa Mataifa Waonya Dhidi ya Kugawanya Dunia 'Katika Pande Mbili'

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa mataifa ya G7 kujiepusha na kugawanya ulimwengu katika kambi za mtindo wa Vita Baridi zinazofungamana na Marekani au China. Wakati huo huo, viongozi hao wa Magharibi walizifanya Urusi na China kuwa kiini cha taarifa ya pamoja kuhusu silaha za nyuklia. Akizungumza na gazeti la Kyodo News la Japan wakati viongozi wa Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani walipokutana Hiroshima siku ya Jumamosi, Guterres alitoa wito wa "mazungumzo na ushirikiano hai" kati ya mataifa ya G7 na China kuhusu masuala ya hali ya hewa. mabadiliko na maendeleo. "Ninaamini ni muhimu kuepuka mgawanyiko wa dunia kuwa mbili, na ni muhimu kuunda madaraja ya mazungumzo ya dhati," alisema.

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Marekani yajitoa katika mkataba wa nyuklia wa enzi za vita vya baridi na Urusi Rais Vladimir Putin na Donald Trump, katika picha ya mnamo 2017 Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya. Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500. ' Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana. Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani. Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake Rais Donald Trump m...

KOREA KASKAZINI YA TOA ONYO KALI KWA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya Korea kaskzini ilirusha makombora yake mawili katika bahari ya Japan Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini. Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini. Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja. Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora. Matamshi ya bwana Kim yalioripotiwa katika vyombo vya habari yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao. Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo. Ijapokuwa ...

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake

John Bolton amepewa jukumu la kupanga jinsi ya kuniangamiza' Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akizungumza na wanahabari mjini Caracas Desmba 12,2018 Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amedai kuwa Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake. Amewaambia wanahabari kuwa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani John Bolton, anahusuka moja kwa moja na njama hiyo japo hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo. Rais Trump amemtaja Maduro kama kiongozi wa kiimla na kumwekea vikwazo. Mapema wiki hii maafisa wakuu wa Urusi na Marekani walijibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumatatu katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Madur...