Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Marekani yajitoa katika mkataba wa nyuklia wa enzi za vita vya baridi na Urusi




Rais Vladimir Putin na Donald Trump, katika picha ya mnamo 2017

Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya.

Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987.

Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500.

'


Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana.

Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani.


Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Rais Donald Trump mnamo Februari ametangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye.

Kuna hatari gani?

"Breki ya thamani katika vita vya nyuklia" inaeleka kupotea, ameonya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres.

"Huenda hili likaongeza na sio kupungua tishio la makombora," aliongeza, na kuomba pande zote kutafuta "makubaliano mapya ya mtazamao wa pamoja ya udhibiti wa silaha kimatiafa".

Wachambuzi wanahofia kwamba kutibuka kwa makubaliano hayo ya kihistoria huenda kukachangia ushindani mpya wa silaha kati ya Marekani, Urusi na China.

"Kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo sasa, tutashuhudia utengenezaji na utumiaji wa silaha mpya," Pavel Felgenhauer, mchambuzi wa zana za Urusi ameliambia shirika la habari la AFP. "Urusi tayari ipo tayari."

Mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameiambia BBC kuwa makombora ya Urusi - ambayo alisema kuwa ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba huo" - zina uwezo wa nyuklia, ambayo ni magumu kutamabua na yanaweza kufika katika miji ya Ulaya katika muda wa dakika.



"Hili ni jambo zito," aliongeza. " Mkataba wa INF umekuwa jiwe la msingi katika udhibiti wa silaha kwa miongo kadhaa, na sasa tunashuhudia kuvunjika kwa mkataba huo ."

Ameongeza kwamba hakujakuwepo "ishara zozote" kuwa Urusi itatii na makubaliano hayo na kwamba "ni lazima tujitayarishe kwa ulimwengu usiokuwa na mkataba wa INF na ulio na makombora zaidi ya Urusi".

Stoltenberg pia alisema kuwa uamuzi wowote wa Nato kuhusu namna gani ya kujibu utatolewa baada ya kupita muda huo wa mwisho uliotolewa.

nato haina mpango wa kutuma makombora yake ya ardhini Ulaya lakini makombora ya angani na ya ulinzi, ya mazoezi na utayari wa vikosi vyake na mipango mipya ya udhibiti wa silaha huenda yakawa ni sehemu ya jibu lake.

Mkataba wa (INF) ni nini?


Kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev na rais wa Marekani Ronald Reagan walisaini mkataba wa INF mnamo 1987

Ulisainiwa na Marekani na uliokuwa Muungano wa Sovieti mnami 1987, mkataba huo ulipiga marufuku silaha zote za nyuklia na makombora yasio ya nyuklia ya masefu marefu na ya wastani isipokuwa ya baharini.


Marekani ilikuwa na wasiwasi kuhusu kutumwa kwa kombora la SS-20 la Sovieti mnamo 1979 na ilijibu kwa kuweka makombora ya masafa mafupi ya ardhini Ulaya - hatua iliyozusha maandamano makubwa.


Kufikia 1991, takriban makombora 2,700 yaliharibiwa.


Mataifa hayo mawili yaliruhusiwa kukagua hifadhi za taifa mwenza.


Mambo yaliharibika wapi?

Mnamo 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kuwa mkataba huo haushughulikii maslahi ya Urusi.

Hilo lilifanyika baada ya rais wa Marekani George W Bush, mnamo 2002, kuitoa Marekani katika mkataba wa kupinga makombora ya masafa ya juu, uliopiga marufuku silaha zilizoundwa kuzuia makombora ya aina hiyo.

Mnamo 2014, rais wa wakati huo Marekani Barack Obama aliishtumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo wa INF baada ya kutuhumiwa kufanya majaribio ya kombora la ardhini.


Urusi inakana kuunda silaha zinazokiuka mkataba huo

Inaarifiwa aliamua kutojitoa katika mkataba huo chni ya shinikizo la viongozi wa mataifa ya Ulaya, waliosema hatua kama hiyo huenda ikachangia ushindain wa umiliki wa silaha.

Alafu mwaka jana, Nato ikaunga mkono tuhuma za Marekani na kuishutumu rasmi Urusi kwa kukiuka mkataba huo.

"Washirika wamehitimisha kuwa Urusi imeunda na kutumia kombora 9M729, hatua inayokiuka mkataba wa INF na kuzusha hatari kwa usalama kati ya Ulaya na Atlatiki," taarifa kutoka mawaziri wa mambo ya nje wa Nato imeeleza.

taarifa hiyo imesema mataifa wanachama "yanaunga mkono" tuhuma za Marekani kuwa Urusi inakiuka mkataba huo, na kuoa wito kwa Moscow "irudi kutii kwa dharura na kikamilifu mkataba huo".

Urusi imekana tuhuma hiyo na rais Putin amesema ni kisingizio kwa Marekani kujito akatika mkataba huo.

Huku uhusiano kati ya Washinto na Moscow ukizidi kudorora, Uturuki mwezi uliopita ulipokea sehemu ya kwanza ya mfumo wa kombora la ulinzi S-400 licha ya upinzani kutoka Marekani.

Marekani imeonya kuwa Uturuki haiwezi kumiliki kwa pamoja mfumo huo wa S-400 na ndege za kivita za Marekani aina ya F-35.

Uturuki na Marekani sio washirika wa Nato lakini Uturuki imekuwa ikiidhnisha ushirikiano wa karibu na Urusi.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...